Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Monday, October 14, 2013

JAY Z ALIVYOJICHANGANYA NA RAIA KWENYE TRENI:

 PICHA/Story TimesFm
Unaikumbuka ile surprise ya Mheshimiwa Mwakyembe kujichanganya kwenye treni ya abiria bila kutoa taarifa? Eeh..sasa Jay Z naye amefanya yake japo malengo yao yanatofautiana.
Rapper mwenye utajiri mkubwa na ulinzi wa kutosha amewasuprise fans wake wa London baada ya kujichanganya nao kwenye usafiri wa treni  wakati anaelekea kwenye tamasha lake katika eneo maarufu kwa burudani na sanaa ‘O2’ lililoko kusini mashariki mwa jiji hilo.
Ripoti toka katika nchi ya Malkia Elizabeth zinasema baba Blue Ivy ambae yuko jijini London ikiwa ni kati ya ratiba ya Magna Carta World tour, jumamosi jioni alipanda treni kama abiria wa kawaida akiwa ameongozana na
Producer Timberland na Chris Martin.
Kwa mujibu wa abiria waliokuwa nae kwenye treni hiyo, Jay Z hakuonesha ustaa tena bali alianza kupiga story na abiria hao kama mmoja kati ya abiria mchangamfu
Moja kati ya fans wake waliokuwa kwenye treni hiyo alitweet “Casually getting on a train with Jay Z, Chris Martin, and Timbaland.” Akaweka na picha inayoonesha Jay Z yuko kwenye Treni. Fans wengine pia waliendelea kutweet kuhusiana na tukio hilo.
Nayo akaunti inayotumia jina la ‘Always Roc Nation’ waliandika, "Jay Z, Chris Martin and Timbaland took the tube to the O2 Arena tonight!”

Imeandikwa na Shakoor Jongo na Musa Mateja.
TOA MAONI YAKO HAPA:

No comments:

Post a Comment