Wakati
wasanii mbalimbali ambao wanaunda kundi la muziki maarufu kama Bongo
Fleva na wale wa filamu wanaojulikana sana kwa jina la Bongo Movie
wakijiandaa na mpambano mkali katika Uwanja wa Taifa wa mpira uliopo Dar
es salaam, siku ya Saba saba katikaTamasha la Tumaini, hali imeshaanza
kuwatisha baadhi ya wasanii katikamakundi yao. Wapo ambao wamepoteza
tumaini kwakuwa hawawaoni wasanii wenzao ambao wamekuwa wakiwategemea
katika michezo yao, na wapo ambao wanasikia wasanii wenzao siku hiyo
watakuwa na show sehemu mbalimbali hao ni katiya wale wa Bongo Fleva,
lakini Bongo Movie wanatamani kuwaona wasanii wa Bongo Fleva wote
wakiwemo na kuwatia aibu kama wao walivyotiwa aibu kwa kupigwa 2-0
katika kuchangia waathirika wa Mabomu wa Gongolamboto. Kilammoja na hamu
yake, ila wengine hofu ya kutoneshwa vidonda kwa kupigwa magoli mengine
na kuyarudia matokeo ya mwanzo
|
Kaka wewe ni mkaaaaaali sn kumbe!!dah!!sijaamin
ReplyDelete..yaani unapiga namba 3 km robert carloss wa brazil enzi zile