MSANII
CHIPUKIZI WA HIP HOP TOKA PANDE ZA MWANANYAMALA KWA MAMA ZAKARIA….AMEACHIA PINI
3 ZA NGUVU HIVI PUNDE TU, MSANII HUYO
CHIPUKIZI NI MOJAWAPO YA WASANII WANAOKUJA
JUU KWA KASI KWENYE GAME YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA……”SIDE FUNDI “ KAMA ANAVYOJULIKANA NA
MASHABIKI WAKE AMEKAMILISHA HIZO PINI 3
KATIKA STUDIO 2 TOFAUTI………… WIMBO WA KWANZA UNAITWA “MR. POLITICIAN” AMBAO AMEFANYIA KATIKA STUDIO ZA VISION CHINI YA
PRODUCER FREEZA NA NYIMBO ZAKE MBILI
ZILIZOBAKI AMEFANYIA KATIKA STUDIO YA
AG`S RECORD CHINI YA USIMAMIZI WA MTU MZIMA LAZARO. SIDE FUNDI ANASEMA KUWA
KIBAO CHAKE CHA “MR. POLITICIAN”
NDICHO KIBAO AMBACHO YEYE MWENYEWE ANAONA KITAFANYA VIZURI KWENYE DURU LA
MUZIKI KWA SASA!....... WIMBO HUO
AMEZUNGUMZIA ZAIDI KUHUSU MAISHA YA KAWAIDA YA MLALAHOI, VIJEMBE,
KEJELI, KARAHA, SHIDA ZA UMASKINI KWENYE
JAMII, SIASA NA VITUKO VYA VIONGOZI WETU
KILA KUKICHA. HAKIKA WIMBO HUU UTAKUWA GUMZO MTAANI. UKIACHA WIMBO HUO WA MR. POLITICIAN, SIDE
FUNDI ANA NYIMBO ZINGINE 2 AMBAZO NI “SAUTI
YANGU” NA NYINGINE INAITWA “WANAKOSA RAHA”. SIDE FUNDI ANAKAZIA KUWA WIMBO ZAKE ZA HIP HOP AMBAZO
ZINAZUNGUMZIA MAISHA HALISI YA MTANZANIA HASA YA WALE WALALAHOI HAKITETEA HAKI
ZAO AU VILIO VYAO VISIKILIZWE NA VIONGOZI WETU WA NGAZI ZA JUU……KWA KUTUMIA MUZIKI
NAAMINI KUWA KILIO CHA MLALAHOI KITAKUJA SIKIKA KWA VIONGOZI AMBAO WANAZIBA
MASIKIO HUKU ILI HALI MATATIZO KWENYE JAMII
YANASHINDWA KUTATULIWA…………….HUYO NDIO SIDE FUNDI………. AU SAUTI ILIYO KIZANI…!!!!! |
No comments:
Post a Comment