Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Saturday, August 31, 2013

HIZI NDO SABABU ZA AUNTY EZEKIEL KUPIGWA CHUPA CLUB BILICANAS:

Jumapili iliyopita katika ukumbi wa bilicanas mwanadada, Aunty Ezekiel alipigwa chupa na kujeruhiwa vibaya na mwanadada aliyetambuliwa kwa jina la Ivony Bigirwa katika show ya muziki ambapo wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliopo chini ya kampuni  ya Wema Sepetu ya Endless fame walikuwa wakitambulisha nyimbo zao mpya
Chanzo nini?

Baada ya kufuatilia kwa karibu na kuichunguza habari hii bongomovies tumegundua kuwa chanzo kilikuwa ni ‘beef’ la kugombania mwanaume ambaye anasadikika ni mume wa mtu kati ya mwanadada huyo (Ivony) na Aunty Ezekiel
Ilikuaje?


Mpashaji wa habari hii anasema kuwa wanadada hao walikuwa ukumbini hapo na ghafla mwanaume huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la Sunday alitokea ukumbini hapo na ndipo patashika hilo likazuka kila mmoja akidai kuwa jamaa huyo ni wa kwake.
Baada ya vuta nikuvute ndipo uzalendo ukamshinda mwanadada ivony na kuanza kuzichapa na Aunty kabla ya kuamua kuchukua chupa na kumpiga nayo na kumjeruhi maeneo ya mkononi
Hali ya Aunty Ezekiel
Kwa sasa hali yam dada huyu iko vizuri na mpaka tunavyoripoti sasa, habari zinasema amesharuhusiwa kutoka hospitalini kwenda kupumzika nyumbani.
STORY imetoka BONGOMOVIE.COM
TOA MAONI YAKO HAPA:

No comments:

Post a Comment