Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Saturday, August 31, 2013

BONDIA FRANCIS CHEKA ATAWAZWA KUWA BINGWA WA NDONDI DUNIANI:

IMETOKA GAZETI LA HABARI LEO:
BONDIA bora nchini, Francis Cheka ametawazwa kuwa bingwa wa dunia katika uzito wa kati, baada ya kumpiga bondia wa Marekani, Phill Williams katika pambano lililochezwa usiku wa kuamkia jana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa mchezo huo. Ubingwa huo unatambuliwa na Shirikisho la Ndondi Duniani (WBF).
Cheka alipanda ulingoni saa 5.30 usiku, akifuatiwa na Williams dakika sita baadaye na ilipofika saa 5.38, mgeni rasmi wa mpambano huo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete, alipanda ulingoni na kuwasalimia mabondia hao.
Akizungumza baada ya kutambulishwa kwa mabondia hon, Dk Mukangara mbali na kuwatakia heri, alimtaka Cheka kupambana kwa lengo la
kulitetea Taifa, na ilipofika saa 5.45 pambano hilo lilianza.
Katika pambano hilo la raundi 12, lililochezeshwa na refa kutoka Afrika Kusini, Drake Ribbinck, lilianza kwa raundi ya kwanza kupotea kutokana na mabondia wote kuonekana kusomana huku kila mmoja akirusha ngumi za ‘hapa na pale’.
Huku akishangiliwa na mashabiki waliojitokeza katika ukumbi huo, kuanzia raundi ya tatu, nne, tano, saba, Cheka alionekana kumrushia makonde Williams huku akijaribu kukwepa kwa umakini baadhi ya makonde yaliyokuwa yakielekezwa upande wake.
Kimsingi, mabondia hao walionekana kuwa nguvu sawa isipokuwa kwa baadhi ya raundi ambazo Cheka aling’ara dhidi ya mpinzani wake hadi pambano lilipomalizika na Cheka kutangazwa bingwa kwa pointi.
Cheka ambaye pia ni bingwa wa Afrika wa IBF, amefikisha rekodi ya kucheza michezo 29-7, akishinda sita kwa Knockouts, mpinzani wake huyo ana rekodi ya 12-5, akishinda mapambano 11 kwa KO.
Mpambano huo ulioandaliwa na Kampuni ya Hall Fame Boxing & Promotions na kupewa jina la ‘Usiku wa ubingwa Tanzania,’ pia lilishuhudiwa na mapambano matatu ya utangulizi yaliyowakutanisha Mada Maugo dhidi ya Thomas Mashali, Alphonce Mchumia Tumbo dhidi Chupa Chipini na Deo Njiku dhidi ya Alan Komote.
Katika mapambano hayo, Maugo alipigwa kwa pointi dhidi ya Mashali kuwania mkanda wa Afrika uzito wa ‘supermiddle’, Njiku akipigwa kwa pointi na Komote na Mchumia Tumbo akimpiga Chipini kwa KO.
Aidha, ukumbini humo kuliibuka mchezo wa baadhi ya mabondia kugomea mapambano wakishinikiza kupewa malipo yao kabla ya kupanda ulingoni, hatua iliyosababisha mara kwa mara muda kupotea.
Mabondia waliogomea kupanda ulingoni kwa madai hayo ni Mchumia Tumbo pamoja Mashali, lakini baada ya majadiliano ya mapromota, walimaliza suala hilo na kupanda ulingoni.
TOA MAONI YAKO HAPA:

No comments:

Post a Comment