Leo wasanii wa filamu nchini walikusanyika pamoja katika semina maalum
ambayo ilikuwa ikitolewa na Shirika la Hifadhi ya mfuko wa kijamii la
NSSF. Mkurugenzi uendeshaji wa kampuni hiyo Crescentius Magori, alisema
shirika hilo limeamua kufanya hivyo baada ya kugundua Watanzania wengi
wakiwemo wasanii ambao hawajaajiliwa wamekuwa wakikosa fulsa ya kujiunga
na mfuko huo. Alisema mara nyingi watu walioajiliwa ndiyo wamekuwa na
nafasi kubwa ya kupata huduma zitolewazo na mfuko huo ikiwemo huduma ya
matibabu, kiinua mgongo na huduma zingine ambazo zinatokana wanachama wa
mfuko huo. Aidha alisema lengo la mfuko huo waajiliwa na wasiokuwa
waajiliwa kuweza kupata huduma hiyo, lakini mwamko umekuwa mdogo sana
kwa watu waliojiajili.
 |
Swebe pamoja na Sudi |
 |
Recho |
 |
Raisi wa shirikisho akiongea Mwakifwamba |
 |
Maya |
 |
Batuli |