MSANII
maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata dhamana
leo baada ya kukidhi masharti aliyowekewa na mahakama.
Dhamana hiyo imetolewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya hoja za mawakili wanaomtetea kukubalika.
Masharti
aliyokuwa amepewa ni pamoja na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali
wenye kiasi cha Sh. milioni 20 kila mmoja na kuwasilisha pasi ya
kusafiri ya msanii ili kutotoka nje ya nchi hadi kesi hiyo
itakapokamilika.
Huku mashabiki wake na baadhi ya wasanii wenzake wakiwa na furaha mahakamani hapo, kila mmoja alisikika akisema Mungu mkubwa.