Wasanii wa filamu leo kwa pmaoja walikutana katika viwanja vya Leaders
Cloub kujadili juu ya hatma yao na maslahi yao katika tasnia hiyo na juu
ya watu wanaobani Cd za filamu zao na kuuza kama njugu. Pia makundi
mawili ambayo yalikuwa yakikizana siku zote kati ya kampuni inayojiita
Bongo Movie chini ya mwenyekiti Jb na shirikisho la filamu nchini chini
ya Saimon Mwakifamba, wamemaliza mgogoro wao huku kila mmoja akiweka
ahadi kwa mwenzake kwamba anatambua uwepo wake. Miongoni mwa migogoro
ambayo ilifanya mpasuka huo kuwa mkubwa pale Mwakifamba alipofika kwenye
Tv fulani na kutangaza kwamba Bongo Movie haitambui kwa mujibu wa
sheria, huku akianika baadhi ya picha zinazoashiria kundi la Bongo
Movie kwamba ndilo linaua tasnia kwa kufanya umalaya. lakini siku ya leo
tofauti zote hizo waliziweka chini, na kuibua hoja mpya kwamba ni jinsi
gani wanaweza kupambana na maharamia ambao wanadurufu kazi za wasanii
na kuwafanya wawe mafukara daima. Miongoni mwa matukio ambayo
walikubaliana kuyafanya ni kufanya maandamano makubwa yakiongozwa kwa
kuvaa Tisheti, za kuashiri kupamba na uadui huo wa kudurufu kazi za
wasnii. Huku wasnii mbalimbali wakitoa dau ili kukamilisha maandamano
hayo, miongoni mwa watu waliotoa michango yao ni Cloud 112 alitoa
shilingi elfu 50, na usafiri wa kuelekea kwenye maandamano, Jb altoa
laki moja, Tues Kinagala alitoa shiling laki moja na mengine wakasema
watajua na kampuni yake cha kufanya, Dk Cheni alisema yeye atatoa
usafiri, wakati wakubwa wao na wasambazaji wakubwa hapa nchini STEPS
ENTERTAIMENT wakitoa ofa kwamba yoyote atayefanikisha kupatikana kwa
mwaharamia mmoja basi atachukua donge nono la MILIONO MBIL . Kazi hiyo
vijana wa mjiniii |
No comments:
Post a Comment