BENDI ya dansi nchini ya Mapacha Watatu, kuondokewa na
mwanamuziki wao Kalala Junior, wameachai wimbo mpya wa Ona Naonewa huku
wakijiandaa na ujio wa albamu yao ya pili.
Mmoja
wa wanamuziki wa bendi hiyo Jose Mara, alisema kwamba wimbo huo wamemshirikisha
Ali Kiba pamoja na Kharidi Chokoraa utakuwa kwenye albamu hiyo ambayo itakuwa
na nyimbo 7.
Aidha
alisema kwamba jina la la albamu hiyo, amemwachia Chokoraa kwakuwa albamu ya
kwanza alishatoa yeye jina, pia alishatuka wimbo kama usio wa baba na huu wa Ona
naonewa.
“Ujue
kupeana nafasini jambo la muhimu, hivyo jina
la albamu hii itatoka katika wimbo ambao atautunga yeye” alisema.
Pia
alisisitiza kusema bendi hiyo, haitachukua mwanamuziki mkongwe kuogopa lawama,
ila itachukuwa wanamziku chipukizi.
No comments:
Post a Comment