Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Tuesday, February 28, 2012

Arsenal yagoma kutumia Fedha zaidi katika usajili ujao


Mtendaji mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis amesisitiza kwamba Klabu haitopagawa kiasi cha kutumia pesa nyigi katika dirisha kubwa la usajili la wachezaji baada ya kutangaza kupata faida ya pauni milioni 49.5(£49.5million ) kwa mwaka siku ya jumatatu.

Faida hiyo, £46.1m imetokana na uuzaji wa wachezaji, ikijumuisha na kumuuza Cesc Fabregas kwa £30m, Samir Nasri kwa 24m na Gael Clichy kwa £7m.

Cloud 112 alilifahamu kama wiki mbili zilizopita ya kuwa Arsene Wenger alipanga bajeti yapata £55m ili kukisuka upya kikosi chake kwa kuongeza wachezaji wapya katika kipindi cha usajili wa majira ya joto ingawa inaonekana kuna uwezekano wa kuwauza baadhi ya wachezaji wake katika kikosi cha sasa hivi.

Mjerumani Mario Gotze na Lukas Podolski wanaonekana kutakiwa zaidi na wenger katika kuongeza makali ya kikosi chake

Target: Mario Goetze    Wanted: Lukas Podolski

pia inaonekana anaweza kuhamishia biashara yake kwa chelsea kumnyakua kinda la Kiingereza Daniel Sturridge na Fowadi ya Anderlecht Matiaz Suarez. Lakini Gazidis amesema klabu itaendelea kuangalia matumizi yao. "Kikubwa ni kuangalia tunafanya nini tukiwa kwenye uwanja", kama alivyosema Gazidis.

No comments:

Post a Comment