Mmiliki wa bendi ya Twanga Pepeta Asha
Baraka, amekana kwamba hakuongea lolote na gazeti lolote kuhusiana na
bendi yake ya Twanga Pepeta la kuhusiana na jinsi inavyoendelea na
ratiba yake katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani Kareem. Asha alisema
hataki kugombanishwa na dini yake, na magazeti kwakuwa yeye ni muislam
kamili. Aidha amesema yanayoandikwa kwenye magazeti hayo, yeye wala
hausiki na hajawahi kuongea, kwani anaamini atakapoongelea suala hilo
atakuwa anakiuka maadili. Mwisho amedai kwamba hayo yote atakuja
kuongelea baada ya mfungo wa Ramadhani Kareem huu kuisha.
MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment