Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Thursday, November 21, 2013

EXCLUSIVE KUHUSU MINI ZIFF 2013 NA FILAMU ZA BONGO:

MINI ZIFF 2013 inafanyika sambamba na Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tamasha hili dogo litafanyika tarehe 10 -12 Jan, 2014 na kama kawaida ZIFF itatoa tuzo 10 za Filamu kwa waliofanya vizuri kwa mwaka 2013 katika filamu za Kiswahili (Bongo Movie). Tuzo zitakazotolewa ni Muigizaji Bora wa Kiume na Kike, Muongozaji Bora, Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji anayechipukia, Filamu bora katika Sauti, Filamu bora katika Hadithi, Balozi bora wa Filamu za kitanzania, Kampuni au mtu aliyetoa mchango mkubwa katika Tasnia hii kwa mwaka huu na Tuzo ya Heshima. Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania peke yake (Bongo movies) ilikuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili ni utangulizi wa tamasha kubwa la ZIFF litakalofanyika 14 – 22 Juni, 2014.

Tuzo zitatolewa baada ya jopo la majaji kupitia kazi zilizoletwa kwaajili ya Mini ZIFF na pia Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume na Kike zitapata kupigiwa kura na wananchi kupitia namba maalum itakayotolewa hapo baadae kupitia Puch Mobile na hivyo kufanya watu wote Tanzania nzima kupiga kura.
Mini ZIFF itaonesha filamu kwa siku mbili na siku ya mwisho Tuzo zitatolewa kwa walioshinda, pia tunategemea kuwaalika wasanii mbalimbali maarufu kutoka hapa Tanzania kama JB, Cloud, Steve Nyerere, Ray, Makombora, Simon Mwakifamba, Monalisa, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Lulu na wengine wengi.
Pia tunategemea kufanya show kabambe ya muziki baada ya kutolewa kwa tuzo, wasanii watakaopanda jukwaani watatangazwa hapo baadae. Kwa wale wote wanaotaka kuleta kazi zao basi walete sasa ila ziwe ambazo zimetoka mwaka 2013 tu. Wasiliana na Ibra 0713300997(DAR) au Mohd 0778685676 (ZNZ).
MINI ZIFF 2013 inaletwa kwa udhamini mkubwa wa ZUKU, Push Mobile, Azam Marine, Filamu Central Clouds TV kupitia kipindi cha Take One na Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena.



TOA MAONI YAKO HAPA:

MWANA MUSIKI LINEX KUONEKANA KWENYE FILAMU HII:

Msanii Linex Sunday Mjeda aka The V.O.A ameamua kufungua ukurasa wa pili wa kipaji ambacho hajawahi kukionesha cha uigizaji, hivi karibuni ataonekana katika filamu mpya ya muigizaji wa bongo movie Aunty Ezekiel inayoitwa ‘MWAJUMA’.
Kwa mujibu wa tovuti ya bongo5, linex ameeleza kuwa  filamu ya Mwajuma inahusu mwanadada aliyekuwa na maisha ya chini akiwa mama ntilie na baadae kuja kufanikiwa na kuanza maisha ya kihuni hususani kubadilisha wanaume kama nguo
Filamu hii inatarajiwa kutoma mwishoni mwa mwezi ujao


TOA MAONI YAKO HAPA:

Thursday, November 14, 2013

WEMA AWAPONDA WALIO KACHA MSIBA WA BABA AKE, ASEMA SIO WOTE NI:

Kupitia kipindi chake cha ‘In My Shoes’ cha jana, Wema Sepetu alieleza jinsi alivyojisikia baada ya baadhi ya waigizaji wenzie wa Bongo Movie kugoma kuhudhuria msiba wa baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, mwishoni mwa mwezi uliopita kwa madai kuwa yeye hakuwa akifanya hivyo kwenye misiba mingine.
“Imeshatokea, wameacha kuja kwenye msiba, ni wao,” alisema Wema. Sio Bongo movie nzima, ni baadhi tu ya watu ambao wanauelewa na upeo mdogo ambao waliamua kutokuja. Lakini niliona Bongo movie wengi, walikuwepo marafiki zangu wengi, akina Batulli, akina Esha, Wolper alikuja, Lulu, JB alikuja, Jokate alikuja, Adam Kuambiana alikuja. Ambaye napenda nimpe my special thanks and appreciation, ambaye alijitolea from the beginning wa msiba mpaka to the end ni Dokta Cheni kwakweli. Dr Cheni, I thank na ntazidi kumshukuru,” alisema.
“Marafiki zangu kama akina Kajala, akina Zamaradi, wale sio marafiki, wale tayari ni ndugu, kwahiyo siwezi kuwaweka kwenye appreciation wala kwenye thanks.”
Katika kipindi hicho pia, Wema alisema yeye na ndugu zake walijua kuwa baba yako ni muumini wa dhehebu la Roman Catholic siku chache kabla ya kufariki dunia.
Balozi Issac Abraham Sepetu (71), alizikwa kikristo katika kijiji cha Mbuzini,mkoa wa Kusini Unguja October 30 ambapo mazishi yake yalihudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohammed Shein pamoja na viongozi wengine. br />


TOA MAONI YAKO HAPA:

Tuesday, November 12, 2013

SABABU ZA IRENE UWOYA KUJIFUA MAZOEZI KWA MATUMLA.

MSANII wa filamu wa kike Bongo Irene Uwoya yupo katika maandalizi ya kuanza mazoezi ya ngumi baada ya kumpata mwalimu ambaye ni Bondia maarufu Rashid Matumla ‘Snake Boy’ akiongea na FC Irene kasema kuwa ameamua kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiweka vema na kulinda nafasi yake ya uigizaji kwani amegundua wasanii wengi wanapoteza mvuto kwa kujiachia kwa unene.

“Nimejipanga kwa kufanya mazoezi ya nguvu chini ya mwalimu wangu Rashid Matumla na nipo fiti kwa ajili ya kujifua najua kuigiza ndio ajira yangu lakini nikijiachia na kunenepa bila mpango nitaanza kucheza nafasi za akina bibi muda si mrefu na najiona mwili
unavyoninyemelea sitaki manyama uzembe,”anasema Irene Uwoya.
Irene ni moja kati ya wasanii wakali wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamau Bongo huku pia akiwa ni moja kati ya watayarishaji wa filamu wanadada akiwa ameandaa filamu la Apple filamu iliyotengenezwa kwa gharama kubwa na kuwashirikisha wasanii kama Patcho Mwamba, Baba Haji na wasanii wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo.


TOA MAONI YAKO HAPA:

Monday, November 11, 2013

JACQUELINE WOLPER AFUNGUKA BAADA YA KUBADILI DINI KWA MARA YA PILI;

Hatimaye mwanadada Jacqueline Wolper ameamua kuweka wazi kilichotokea mpaka kuamua kubadili Dini yake ya Uislamu na kurudi kwenye ukristo tena. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa bongo movies ametoa ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake.
“…mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza nakuwaelewesha mashabk zangu stak maswal nawapenda wote…”
Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena baada ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.
Swali ni je, atabadili dini tena akitokea mwingine wa dini aliyo tofauti na sasa? br /> (imetoka Bongomovies)
TOA MAONI YAKO HAPA:

Saturday, November 9, 2013

TUSIMLAUMU RAY,WEMA ALIKUA HAJITOI KWENYE MISIBA YA WENZAKE;''STEVE NYERERE''

Tusimlaumu Ray; Wema alikuwa hajitoi kwenye misiba ya wenzake- Steven Nyerere
Msanii wa filamu, Steve Nyerere amesema Wema Sepetu alikuwa hajitoi kwenye matatazo ya wasanii wenzake wa filamu na ndio maana wasanii wengi wa filamu wakashindwa kuhudhuria katika mazishi ya baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu mwishoni mwa mwezi uliopita.

Akizungumza  leo Steve,amesema anawataka watu waache kumtupia lawama Vicent Kigosi aka ‘Ray’ wakati mwanadada huyo alikuwa hahudhurii katika matatizo ya wenzake.

“Mnamlaumu bure Ray jambo ambalo hajafanya kwakuwa Ray ni jalala basi kila kitu mnamtupia,jamani mwacheni apumzike,” amesema Steve.

“Sisi katika Bongo Movie Unity tuna uongozi, tuna mwenyekiti,tuna mwenyekiti wa mipango ambaye ndio mimi, na tuna makamu wa mwenyekiti ambaye ndio mimi na tuna makamu mwenyekiti ambaye ni Irene Uwoya. Lakini sisi taratibu zetu kwenye misiba kama unaona kwenye misiba yetu tunajitoa,lakini linavyotufika tunaangalia ni mwanachama gani naye anakua anajitoa katika misiba ya wenzake