Leo wasanii wa filamu nchini walikusanyika pamoja katika semina maalum
ambayo ilikuwa ikitolewa na Shirika la Hifadhi ya mfuko wa kijamii la
NSSF. Mkurugenzi uendeshaji wa kampuni hiyo Crescentius Magori, alisema
shirika hilo limeamua kufanya hivyo baada ya kugundua Watanzania wengi
wakiwemo wasanii ambao hawajaajiliwa wamekuwa wakikosa fulsa ya kujiunga
na mfuko huo. Alisema mara nyingi watu walioajiliwa ndiyo wamekuwa na
nafasi kubwa ya kupata huduma zitolewazo na mfuko huo ikiwemo huduma ya
matibabu, kiinua mgongo na huduma zingine ambazo zinatokana wanachama wa
mfuko huo. Aidha alisema lengo la mfuko huo waajiliwa na wasiokuwa
waajiliwa kuweza kupata huduma hiyo, lakini mwamko umekuwa mdogo sana
kwa watu waliojiajili.
Nyota wa muziki wa kizazi kipya Matonya, amesema hivi sasa ameamua kuwachukuwa wachekeshaji kwaajili ya kuwafanya Madensa, pindi anapopanda jukwaani kuimba. Alisema anafanya hivyo lengo lake lake likiwa ni kutimiza ahadi yake ya kutoa burudani mbili kwa wakati mmoja. Alisema miongoni mwa stedi shoo wake, ni Kingwendu, na wengine.
wasanii wa filamu nchini ambao wanaunda kampuni ya Nyerere The Power, juzi walikuwa wakisherekea Nyerere Day katika beach ya Sunrise. Katika sherehe hiyo ambayo pia ilionyeshwa filamu ya Mwalimu Nyerere, wasanii waliweza kujiburudisha kwa kuogelea huku kiongozi wa kundi hilo Steve Nyerere akitoa burudani ya kuimba.
MSANII maarufu wa filamu nchini, Hissan Muya ‘Tino’, amesema ,
WALE WENYE VIPAJI WOTE VYA SANAA YA MAIGIZO NA NYINGINEZO ZOTE SIKU YA TAR 26
october KWENYE
UZINDUZI WA TINO ,,,,,TINO MUYA FILMS.... ITAZINDUA MUVIE YA
C,I,D PIA ITAZINDUA RASMI ,,,,,,MUVIE STAR SEACH,,,,YANI M,S,S,,,,,,,NJOO UJUE
UTAAANZIAAA WAPIII KUONYESHA KIPAJI CHAKO,,,,,,,,,,UKUMBI BISNESS PAK VICTORIA
Akizungumza hivi karibuni Tino alisema kuwa kwa sasa amesitisha mpango
wa kutengeneza na kucheza filamu za mapenzi kwa kuwa wengi wamejikita
kutengeneza filamu za aina hiyo na kusahau mambo muhimu yanayoigusa
jamii hasa janga kubwa la ukimwi, njaa na mengine mengi.
Tino alisema sababu nyingine ya kuzitosa filamu za mapenzi ni baada ya
kutengeneza filamu ya ‘Shoga’ na baadaye kubadilishwa jina na kuitwa
‘Shoga yangu’ iliyokuwa na lengo la kuelimisha jamii kuhusu suala zima
la ushoga, badala yake ikaja kumletea matatizo.
Nyota wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini ambao wanawania tuzo za Channel O, Ambewe Yesaya 'Ay' na Cpwaa, wamezindua video maalum kwaajili ya kuhamasisha upigaji wa kula katika tuzo wanazowania nchini afrika kusini.
Cpwaa akitoa maelezo ya kutosha jinsi ya kuwapigia kula.
Wakati tunarudi kutoka shooting Bunju tulipofika katika eneo la Mbezi na Africasana, tumekuta nyumba ikiungua moto. Kujenga nyumba ya ghorofa kuna raha yake na karaha yake, kwani watu wengi walikuwa wamejaa lakini walishindwa kutoa msaada kutokana na nyumba hiyo kuwa ya ghorofa, hata magari ya Fire yaliyofika hapo yalitoa masaada mdogo sana katika kuhakikisha wanazima moto huo.
Ile filamu ambayo ilikuwa ikisubiriwa na watu wengi yenye histori ya Kipekee ya Fungate, imeingia sokoni hivi karibuni. Katika filamu hiyo ambayo imeongozwa na Kampuni ya CY & CL Company, imewashirikisha wasanii kibao akiwemo Liberty Msuya, Issa Mussa 'Cloud 112', Batuli na wengine kibao
Naitwa Issa Mussa 'Cloud112' karibu kwenye blog yangu, ambayo nitakuwa nikikuleteeni stori mbalimbali zikiwemo za filamu zangu zinazokuja na zilizopita, na za watu wengine karibuni sana.