Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Tuesday, October 29, 2013

RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU MZEE SEPETU NILIYOIPATA:

RAY:
Habari zenu ndugu zangu, i hope mmeamka salaama salamin, kwa wale wagongwa allah atawaafu inshaallah:
Tangu juzi nimekua nikishare na nyinyi taarifa za Msiba wa Baba Mzazi wa Mwanafilamu mwenzangu WEMA SEPETU mzee ABRAHAM SEPETU:
Taarifa hizi nazipata kutoka kwa Ndugi wa Karibu wa Wema Sepetu ambae ni Binamu yake anaeitwa RAY ambaye ni Mkurugenzi wa Bendi ya Cococnut Zanzibar;
Ratiba YA Mazishi yatakavyo kua Kisiwan Zanzibar:
PICHA YA MAREHEMU ABRAHAM SEPETU ENZI ZA UHAI WAKE:
''Maiti itaondoka na Boti ya Kesho Asubuhi kuelekea Zanzibar na Kufikishwa Moja kwa moja kanisani kwa misa fupi kisha baraza la wawakilishi la Zamani, kwa waheshimiwa kutoa heshima zao za mwisho.Baada ya hapo msafara utaelekea nyumbani kwake Mbuzini kwa ajili ya Mazishi:''
kama kuna chcochote kitakacho badilika tutajulishana hapa hapa:
Ahsanteni Endelea kutembelea blog hii na Uwaambie wengine pia:
R.I.P Mzee Abraham Sepetu
TOA MAONI YAKO HAPA:

Sunday, October 27, 2013

TAARIFA JUU YA KIFO NA MAZIKO YA BABA WA WEMA SEPETU (MZEE ISSAC SEPETU)

Leo mapema tumepokea taarifa za kifo cha Baba mzazi wa Msanii nguli wa Filam nchini Tanzania Wema Sepetu Mzee Issac Sepetu (pichani), Ambae alikua anaumwa na amelazwa katika hospitali ya TMJ jiji Dar,Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Band Ya #COCONUT BAND ya Zanzibar Bwana RAY ambae ni  ndugu na wema sepetu ba mkubwa kwa ba mdogo, alisema mwili wa mzee sepetu kwa sasa umeshapelekwa katika Monchwari ya hospital Kuu ya Muhimbili:
Alipotakiwa kusema kuhusu wapi na nilini atazikwa mzee huyo: Bw; Ray alisema
Ray Mkurugenzi wa Coconut Band Zanzibar:
''kwa sasa tunawasubiri baadhi ya watoto wake waliyokuwepo marekani wafike, na wengine waliyokuwepo ujerumani na tunatarajia watafika kwenye jumanne, sasa wakifika tutazika kati ya juma nne au juma tano, na mzee tunatarajia atazikwa kwenye shamba yake Visiwani Zanzibar iliyoko shamba Mbuzini''
TOA MAONI YAKO HAPA:

Wednesday, October 23, 2013

(VIDEO) TRAILER FILAMU MPYA YA CLOUD 112 ''DR MAX''

Tumshkuru muumba kwa kutujaalia kumaliza salama kile ambacho mlitutuma kukifanya Timu nzima ya CY & CL COMPANY  Tmemalizaq kwa salama na Amani sasa imebakia zamu yenu tuu kukiangalia kile ambacho tulikua tunakifanaya, Filam Yetu ya DR MAX imemaliza Licha ya changamoto za hapa na pale, 
kua wa kwanza angalia hapa Trailer ya Filamu hii hapa pekee, then utatupa comment yako hapo chini:#
ASNTENI kwa Kuwa na sisi mpaka leo kwa support zenu: asanteni sana angalia hapa Trailer;
 
TOA MAONI YAKO HAPA:

ANGALIA HAPA SEHEMU YA KWANZA YA KIPINDI CHA WEMA SEPETU

Kile kipindi kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa filamu nchini , “Wema Sepetu Reality show” kwa mara ya kwanza kimeruka hewani kupitia kituo cha TV cha EATV  hapo jana.
Katika episode hii ya kwanza, Wema amejitambulisha nan  kuelezea historia yake kwa ufupi kukusu yeye.

TOA MAONI YAKO HAPA:

Monday, October 21, 2013

Tughe wataka Zitto achukuliwe hatua kwa kutaja mshahara wa rais

 (HABARILEO)
HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu, imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) kulaani hatua hiyo na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa vile ni ukiukaji wa sheria.
Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.
Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Ally Kiwenge alisema Dar es Salaam jana kwamba pamoja na hatua hiyo kukiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini inayosema mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa, pia kitendo hicho si ajenda ya wafanyakazi hivi sasa.
Alisema ajenda ya wafanyakazi kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana kufa kupona katika kuhakikisha kuwa mshahara wa mfanyakazi unaongezeka kukidhi mahitaji ya mwezi mzima na kuwaondolea mzigo wa mikopo inayowaandama.
“Huu si wakati wa wafanyakazi kutaka kujua mishahara ya Rais au Waziri Mkuu, ajenda yetu kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi ili ukidhi mahitaji muhimu tofauti na sasa,” alisema Kiwenge.
Alisema pamoja na hilo ni mkakati wa wafanyakazi sasa kuona wabunge wanatumia muda wao uliosalia kabla ya Bunge kuvunjwa kuhakikisha mambo makubwa mawili yanaingizwa katika Katiba mpya, moja ikiwa ni nafasi ya mfanyakazi kikatiba ikoje na pia kuona Katiba mpya inasema nini juu ya hatima ya maslahi ya wafanyakazi.

KIANGALIE KIKOSI CHA YANGA KITAKACHO IVAA SIMBA LEO:

Kama tujuavyo leo kuna mechi kali sana kati ya wapinzani wa jadi, SIMBA na YANGA, ahadi kede kede zimewekwa na wachezaji pamoja ana mashabiki wa timu hizo mbili, majigambo pia tumeyasikia kutoka kwa wachezaji pamoja ana mashabiki wa timu zote mbili, lakini tunavyoamini sisi ni kwamba mpira Dakika tisini,Kabla hujafika hebu chukua time kuangalia list ya YANGA, itakayoingia uwanjani pamoja na Reserve wake hapa:

Friday, October 18, 2013

WASTARA AUMIA MGUU TENA NAIROBI:

Na Gladness Mallya(gpl)
MWANADADA anayeendesha maisha yake kwa kuuza nyago kwenye filamu Bongo,  Wastara Juma ameumia mguu baada ya kuwekewa mwingine mpya wa bandia huko Nairobi nchini Kenya.

 Akizungumza na paparazi wetu siku chache baada ya kurudi Bongo, Wastara alisema aliumia wakati akifanya mazoezi ya mguu mpya aliowekewa ambapo kwa sasa anaendelea kuuguza jeraha hilo na amerudi mara moja kwa ajili ya Sikukuu ya Idd, ikimalizika atarejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.
“Nimeshindwa kula sikukuu mbali na watoto wangu ndiyo maana nikaja mara moja japokuwa siko vizuri kwa sababu niliumia kwenye mazoezi ya kutumia mguu mpya huko Nairobi  na sasa nauguza kidonda lakini baada ya hapo nitarudi tena Nairobi kwa ajili ya matibabu,” alisema Wastara.
TOA MAONI YAKO HAPA:

WADAU WABARIKI NDOA YA WEMA SEPETU, DIAMOND:

Na Shakoor Jongo(GPL)
Wadau na mashabiki wa mastaa wawili nchini, Wema Sepetu wa Bongo Movie na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wa muziki wa kizazi kipya, wamebariki ndoa ya wapenzi hao kwa kusema kuwa ni watu wanaoendana na kutegemeana kwa kiasi kikubwa.

Mwanzoni mwa wiki hii, Wema na Diamond walitupia katika kurasa zao za mitandao ya kijamii picha zao, ambazo zinaonekana zilipigwa eneo moja kwa simu moja na hivyo kuwapa wakati mzuri mashabiki wao ambao walionekana kupendezwa na uhusiano wao na kupendekeza waoane.
“Hii ndiyo couple bomba zaidi ya wasanii Bongo, kwa nini msioane? Mnapendeza sana jamani, ebu Diamond Platnumz achana na Penny bwana, huendani naye kwanza kuna mambo ya

Monday, October 14, 2013

JAY Z ALIVYOJICHANGANYA NA RAIA KWENYE TRENI:

 PICHA/Story TimesFm
Unaikumbuka ile surprise ya Mheshimiwa Mwakyembe kujichanganya kwenye treni ya abiria bila kutoa taarifa? Eeh..sasa Jay Z naye amefanya yake japo malengo yao yanatofautiana.
Rapper mwenye utajiri mkubwa na ulinzi wa kutosha amewasuprise fans wake wa London baada ya kujichanganya nao kwenye usafiri wa treni  wakati anaelekea kwenye tamasha lake katika eneo maarufu kwa burudani na sanaa ‘O2’ lililoko kusini mashariki mwa jiji hilo.
Ripoti toka katika nchi ya Malkia Elizabeth zinasema baba Blue Ivy ambae yuko jijini London ikiwa ni kati ya ratiba ya Magna Carta World tour, jumamosi jioni alipanda treni kama abiria wa kawaida akiwa ameongozana na

MAMA DIAMOND AINGILIA PENZI LA DIAMOND, WEMA


Stori: Mwandishi Wetu/Gpl
MAMA mzazi wa mkali wa ngoma ya Number One, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameingilia kati penzi lililofufuka upya kati ya mwanaye na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu.
Habari za chini ya kapeti zilitonya kuwa baada ya kuambiwa na kuoneshwa picha za Diamond akiwa kimahaba na Wema alikuja juu akidai kuwa hamtaki Wema kwa kuwa anamkubali zaidi Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar wikiendi iliyopita, bi’mkubwa huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na kuona picha katika mitandao ya kijamii.
“Kuhusu Nasibu (Diamond) kurudiana na Wema, nasikia tu na kuoneshwa picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa tamko,” alisema

Saturday, October 12, 2013

HAMMY B JAJI MPYA TUSKER PROJECT FAME TPF6:

 By EATV
Waandaaji wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba lijulikanalo kama Tusker Project Fame hii leo limemtangaza jaji mpya wa mashindano hayo kutoka Tanzania.

Kwa mujibu wa Meneja wa Tusker Bi.  Bi Sialouise Shayo amesema kuwa jaji ambaye amechukua nafasi ya Mzee Zahir Zoro ni  Hermes J Bariki Hermy B.

Kwa upande wa mzee Zahir Zoro amesema kuwa amewapitisha vijana wanne ambao ana uhakika wataipeperusha vyema bendera ya Tanzania.


Naye Hermy B ameahidi kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwani ana uzoefu na mashindano hayo kwa muda mrefu.
TOA MAONI YAKO HAPA:

RAMA DEE: NAFASI YA R&B NI KUBWA SANA TANZANIA:

 by TIMESFM
Inawezekana we pia ukawa mmoja kati ya watu wanaoamini kuwa nyimbo zenye temple zinazokimbia sana ndio zinazopendwa zaidi Tanzania, au kama we ni msanii unawaza kuhama R&B ufanye  ngoma inayokimbia kama ya…, lakini Mwimbaji wa R&B Rama Dee yeye anaamini R&B ina nafasi zaidi nchini Tanzania na kwa anashauri usipokee maoni ya marafiki zako tu, ila uangalie pia watu duniani wanasikikiliza nini .
Hit Maker wa ‘Kama Huwezi’amefunguka kupitia kipindi cha The Chat cha Timesfm kinachoendeshwa na Ezden The Rocker kila jumamosi saa nne kamili asubuhi hadi saa sita kamili mchana.
“Nafasi ya R&B ni kubwa zaidi Tanzania, usiangalie tu rafiki zako wanasikiliza nini angalia watu duniani wanasikiliza nini halafu utapata jibu zuri zaidi, kwa hiyo R&B ina nafasi nyingi hata kama haina nafasi labda Tanga, ama labda haina nafasi Bukoba lakini ina nafasi zaidi Dar es Salaam na mikoa mingine na labda nchi nyingine tofautitofauti, kwa hiyo opportunities zipo nyingi sana, na wasanii wapo wengi sana wanafanya vizuri na wanafanya na live band, kama akina Damian, The Voice pia wapo, kwa hiyo mi naamini baada ya labda mwaka mmoja kila kitu kitaanza kutoka na kuonekana .” Amesema Rama Dee.
Wimbo wa Rama Dee aliomshirikisha Lady Jay Dee ‘Kama Huwezi’ umeshika nafasi ya 8 kwenye The Chat Countdown yenye nyimbo 20.

TOA MAONI YAKO HAPA:

Thursday, October 10, 2013

PICHA ZILIZOVUJA ZA WEMA NA DIAMOND WAKIWA MJINI MALAYSIA:

Katika kile kinachoendelea mitandaoni, kuhusia na Stars wawili, waliyowahi kuwa wapenzi hapo awali, ni kwamba eti wamerudiana, japo kua Diamond alishatoa Tamko juzi kwamba hakuna mapenzi ya aina yoyote, yanayo muhisha yeye na mwnadada wema lakin, Ghafla Picha za wawili hao wakiwa Nchini MALAYSIA ambako Diamond alienda kufanya show Kipindi Flan hivi zikaanza kuvuja,
Hebu na wewe pata kuzishuhudia picha hizo ingawa Diamond amesema ni Filam Mpya ambayo amecheza yeye na wema, sasa wewe ndio utakua Jaji: mimi simo::

Wednesday, October 9, 2013

COVER YA FILAMU YANGU MPYA YA DR MAX ICHEKI HAPA:

MAELEZO:
''Filamu ya Dr Max, ni Filamu ya Kitanzania inayomzungumzia Dr Max ambae anaamua Kufuta Hatua Kadhaa alizopiga na Kusonga mbele, Lakini hakumbuki kuawa kusonga mbele bila ya Kufuta Dosari za nyuma ni sawa na kuanza tena Safari ya Kurudi nyuma:'
TOA MAONI YAKO HAPA:

Tuesday, October 8, 2013

HIZI TAARIFA ZA MZEE MAJUTO KUGOMBEA UBUNGE 2015;

 (habari/BongoMovies)
Habari tulizozipata zinasema kuwa gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani 'King Majuto' ametangaza kugombea ubunge kwa 2015.
Muigizaji huyu mkongwe mzee Majuto ametangaza  kugombea ubunge jimbo la Tanga mjini.
Majuto  mwenye umri  zaidi ya miaka 60 ametangaza nia yake hiyo alipohojiwa na Clouds, na akadai atagombea kupitia CCM.
Bado tunamtafuta mzee majuto ili aweze kututhibitishia kama habari hizi ni kwa kweli au la na kama ni kweli ana mipango gani na jimbo hilo la Tanga mjini.
Je, kama ni kweli, unahisi ataweza ? Tupe maoni yako
TOA MAONI YAKO HAPA:

Monday, October 7, 2013

Washiriki wanne wanaoiwakilisha Tanzania kwenye Tusker Project Fame

Tusker project fame mashindano ambayo yamewahi kuwapa ustaa wasanii kama Hemed PHD wa Tanzania yamefikia hatua ya washiriki kukaa kwenye academy ambapo matumaini ya Watanzania kufanya vizuri kwenye mashindano haya yapo mikononi mwa watu wanne.
Watu wenyewe ni  Angel, 23 yrs, Hisia 21 yrs, Tanah 21 yrs na Dubson 25yrs, unaweza kufatilia show ili ujue jinsi ya kuwapa support Watanzania hawa mtu wa nguvu ambao wako kwenye list ya zaidi ya wasanii 15 kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki.


TOA MAONI YAKO HAPA:

BARAFU ATOA YA MOYONI KUHUSU VIPAJI VYA MTAANI:

BY  filamucentral
MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Suleiman Barafu ametoa kali pale alipoongelea soko la filamu la Bongo kwa kuwalaumu baadhi ya wasanii ambao hajawataja majina kwa kusema kuwa wasanii hao wapo katika tasnia ya filamu kwa muda mrefu kiasi cha kuona fani hiyo ni mali yao na hakuna anayestahili kuingia au kuigiza.
“Katika soko la filamu kuna tabia ya kubaniana, wasanii wakongwe hawataki kizazi kipya, kila sehemu wanataka wao pamoja na kuwa hawawezi, unamkuta mtu akipewa nafasi ya kukuongelea kwa bosi anakuponda mwanzo mwisho, sasa na sisi tunasema Maveterani wakae pembeni wasubiri mechi za mazoezi,”anasema barafu.
Msanii huyo ambaye pia ni muongozaji wa filamu amedai kuwa mitaani kuna vipaji vingi lakini vinanyimwa nafasia na wasanii wakongwe ambao hawataki kabisa kutoa nafasi kwa wasanii hao ili kuleta ushindani wa kweli katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Barafu yupo mbioni kuachia filamu yake inayokwenda kwa jina la Dala dala kutoka kampuni ya Usambazaji ya Leo Media.


TOA MAONI YAKO HAPA:

Sunday, October 6, 2013

MATOKEO YA ENGLISH PREMIER LEAGUE :


epl 1
 (story/picha millardayo)
Ligi kuu ya soka nchini England  imeendelea hii leo ambako michezo nane imepigwa .
Katika mchezo wa kwanza Manchester City waliwafunga Everton kwa mabao matatu kwa moja.
Everton walianza kufunga kupitia kwa Romelu Lukaku lakini Mabao toka kwa Alvaro Negredo , Sergio Kun Aguerro pamoja na bao la kujifunga la kipa Tim Howard yaliwapa Man City pointi Zote tatu .

ALBAM YA RAY C YAKAMILIKA RASMIN:

Nguli wa muziki wa Bongo Fleva Rehema Chalamila‘Ray C’amekamilisha albam ya nyimbo zake aliyokuwa akirekodi studio kwa miezi kadhaa.
 Kupitia mtandao wa instragram Ray C alisema kuwa….Album imekwishaaaaaaaaaaaaaaaaaa!Thank You Lord!
 Hivi karibuni msanii huyo alipost video na kuwaonjesha mashabiki wake ladha kidogo kati ya nyimbo zitakazopatikana kwenye albam hiyo ambayo haijajulikana itaitwa jina gani.
TOA MAONI YAKO HAPA:

Friday, October 4, 2013

HAPPY BIRTH DAY MTANGAZAJI WA CLOUD TV ZAMARADI MKETEMA:

Na mimi ningependa kuwa miongoni mwa wale ambao watamtakia Happy birthday Zamaradi Mketema:
Zamaradi Mketema ni Producer & Presenter wa show ya Take one (movie program) ya  Clouds Tv /clouds FM Radio..
HAPPY BIRTHDAY
TOA MAONI YAKO HAPA:

20 PERCENT NA PRODUCER MAN WATER WAYAMALIZA KIHIVI:


Hakika Nyumbani ni Nyumbani tu ...Mwanamuziki 20 Percent ambayo miaka kama miwili iliyopita alikuwa ni tishio katika muziki wa Bongo Flava Hatimae ameamua kujirudi na kuondoa Beef walilo kuwa nalo na Producer wake ambaye ndio alikuwa anamtoa Man Water ...Wawili Hao wamekuwa kwa muda mrefu hawapatani kila mtu akisema mwenzake ndio mbaya ...ila leo wamekutana katika Ofisi za Magic FM na Kumaliza Tofauti zao na Kuhaidi kufanya kazi pamoja tena...20 Percent toka aachane na Producer huyo ameshindwa kabisa kufurukuta katika Game Hilo na kuonekana ameishiwa kabisa....Tunamuombea Arudi tena kama dhamani tupate Burudani Safi toka kwake;

TOA MAONI YAKO HAPA:

Thursday, October 3, 2013

TATOO YA UWOYA YALETA MTAFARUK:

 credit/BongoMovies
Mwanadada Irene Uwoya ammepa maneno ya busara fan wake kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii hivi karibuni.
Tukio hilo lilikuja baada ya fan huyo kwa jina moja la Hellen kumuandikia Irene uwoya kuwa maneno ya kumshauri kuhusu tattoo yake ya mkononi,
kwanza kabisa mwanadada huyo alimwambia Irene kuwa anampenda sana na pili Irene kama mkristo hatakiwi kuwa na hizo tattoo kwani Mungu hapendi, ndipo Irene Uwoya alimpomjibu kuwa Mungu anaangalia moyo na sio mambo mengine:
Hellen: dada nakupenda sana....ila wew n mkristo jmn izo tattoo mungu apend cyo siri yan#irene
Irene Uwoya: Mungu anangalia moyo si tattoo”
Kama hii haitoshi fans wengine nao wakaanza kuandika..(Tukinukuu)
Kulwa: Moyo kwa maana ya matendo,tabia muonekano ama sivyo?
Piere: Hata mm mkristo na Tatoo ninazo anaesema mungu apendi kuna mstari gani kwenye vitabu vyake vitakatifu ilipoandikwa hapendi tatoo
Je ni sahihi kuchora tattoo kama alivyodai Irene au ni knyume na maagizo ya vitabu vya dini? Tupe maoni yako
TOA MAONI YAKO HAPA:

Wednesday, October 2, 2013

WEMA SEPETU KULISHTAKI GAZETI HILI?ANGALIA ALICHOANDIKA:

MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo,Wema Sepetu ameonyeshwa kuumizwa na habari iliyoandikwa na gazeti la udaku la Filamu baada ya kuandika kuwa ameenda nchini China kuuza madawa ya Kulevya‘ unga’na kuandika waraka(ujumbe) mrefu mtandaoni kuwa amechoshwa kusakamwa kila wakati kwa kuandikwa habari za uongo juu yake.

Wema alipost ukurasa wa mbele wa gazeti hilo na kuandika …Hahahahha.. haya niombeeni watanzania.... aisee... magazeti ni noumerrr... mambo ya kunyongwa tena na wakati sufuria zina shake zenyewe... dah... this made my day...…

Tuesday, October 1, 2013

LULU AFUNGUKA YA MOYONI KWENYE SIMINA YA FURSA:


TOA MAONI YAKO HAPA:

IRENE UWOYA AMEACHANA KABISA NA KU ACT FILAM SOMA HAPA ZAIDI:



CREATIT DSTV
Mwigizaji Irene Uwoya ambae alipata tuzo ya Steps kama mwigizaji bora kike 2012/2013 amethibitisha kuacha kuigiza movie kwa sasa ili kufanya kazi ambayo ameianza hivi karibuni.

Namkariri akisema: “Nimeamua kuacha mambo ya movie na kuwaachia wengine, haya maamuzi nimeyafanya kama miezi sita iliyopita… Mara ya mwisho kuigiza ni zaidi ya miezi sita iliyopita pia.”

Irene ambae ni mama wa mtoto mmoja kwa sasa anafanya show ya TV ya kusaidia Watanzania wanaoishi kwenye nyumba ambazo ni mbovu au hazina mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye nyumba.

Ni show ambayo haitahusika ku....