Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Saturday, September 28, 2013

Hadji Adam, apata stashahada ya Sanaa ya maigizo leo toka chuo cha Bagamoyo,


Hongera Hadji Adam, apata stashahada ya Sanaa ya maigizo leo toka chuo cha Bagamoyo, ni mfano wa kuigwa
 (habri/picha na bongomovies)
Mwigizaji Hadji Adam leo amepata Stashahada yake ya maigizo ya drama na filamu toka chuo cha sanaa Bagamoyo mkoa wa pwani.
Katika mahafali hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho Hadji pamoja na wahitimu wengine wamepata zawadi na vyeti mbalimbali toka kwa uongozi wa chuo hicho.
Akizungumza na simu tokeo Bagamoyo alipo sasa Hadji amesema kuwa anajisikia furaha sana kuhitimu mafunzo yake yake hayo na anasema kuwa hapo ni mwanzo tuu na anajiandaa tena ili aendelee na elimu zaidi.
“kwakweli nina furaha sana siku ya leo, namshukuru Mungu nimemaliza salama na natumai nikipumzika nitaendelea na masomo zaidi hapo mwakani” alisema Haji.
Bongomovies.com tunapenda kumpa pongezi za dhati haji kwa hatua hii na tunamtakia kila la kheri katika masomo yake yanayokuja.
TOA MAONI YAKO HAPA:

Friday, September 27, 2013

SALAM ALIZOZIPATA WASTARA KUTOKA KWA MASTAR MBALI MBALI HIZI HAPA:

 Leo ni Birthday ya Mwanadada Wastara Sajuki ambaye kwa nyingine kama si mara ya kwanza tangu afiliwe na mumewe, utamuona kwenye Filamu Yangu mpya ya DR MAX itakayotoka hivi Karibuni: na hapo kwenye picha ni scene moja mimi na yeye:

Wastara mwenyewe amejipongeza kwa kusema...
Happy b/day 2 me""Alhamdulilah namshukuru sana m/mungu kwa kueza kunifikisha katika siku hii mpaka sasa ni mzimah""Namtanguliza yeye kwa kila jambo anisimamie katika maisha yangu""Ameen""""

Batuli:
★★You are the best person of this world, I'm sure this year gonna be your greatest★★★ happy birthday to u★★★ happy birthday to u★★★ Happy birthday dear wastara happy birthdat to uuuuuu★★★Love u Chimamy

Nisha:

Wednesday, September 25, 2013

(PICHA)HIZI PICHA ZA MWISHO BAADA YA KUMALIZA KUSHOOT FILAMU YA DR MAX::

Habari za leo watu wangu pamoja na wadau wakubwa wa blog hii, nitakua mchoyo wa fadhila km sitamshukur allah muumba kwqa kutuwezesha kumaliza salaama kabisa kushoot filam mpya ya cy&cl company inayoitwa DR MAX, Na kwa sasa zimebakia process za kitaalam tuu so kaaeni tayari, tutapeana maelezo lini inatoka rasmi na itazinduliwa wapi , kila kitu kuhusu filamu hiyo na Cloud 112 ni hapa kwenye blog yangu;
Asanteni sana kwa ushikiano wenu wa mawazo na kila kitu NAWAPENDA sana;
Angalia picha hapa za mwisho mwisho mimi na crue nzima ya CY&CL COMPANY.......

(PICHA)RAY KIGOSI KUTOKA NA FILAM HII:




(picha/storyna DJCHOKA)
Super Star wa Bongo Movie nchini Ray Kigosi aka The Greatest sasa yupo kwenye matengenezo ya movie yake mpya ambayo amewashirikisha wasanii wenzake wa bongo movie wakali katika game hili. Katika account yake ya Instagram Ray ameonekana akionyesha picha wakati wakiishuti movie hiyo pasipo kutaja jina la movie hiyo huku akiwaambia mshabiki wake wakae mkao wa kula na kuona ujio wake mwingine.

Hebu onja kidogo picha kadhaa wakati wakishuti movie hiyo hapa...

Tuesday, September 24, 2013

MBAYA WA AUNT AHENYA KORTINI

Yvonne Maximilian akiwa eneo la mahakama.
Stori: Musa Mateja GPL
Hatimaye yule mbaya wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel aitwaye Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa mwigizaji huyo.
Yvonne aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kukamatwa maeneo ya nyumbani kwake Kinondoni-Manyanya..........

Sunday, September 22, 2013

DAY 3: PICHA ZA BEHIND THE SCENE ZA FILAMU YA "DR MAX" HIZI HAPA;

k
Kama kawaida fans wangu tunakutana tena tukiwa wazima wa afya Alhamdulilah, Imani yangu na nyinyi ni wazima pia kwa sababu tuu bado tunavuta pumnzi mpaka dakika hii, Ule muendelezo wa Filamu yangu ya DR MAX bado unaendelea nahizi ni picha nyengne kabisa, kuwa wewe wa kwanza kuziona kabla ya mtu mwengne yoyote ndio kwanza naziweka hapa; Na hii ni DAY 3, tulianza na DAY 1 ,tukaja DAy 2 sasa hii ni DAY 3 , Angalia hapa picha za DAY 3, behind the scene
Karibuni sana:

Saturday, September 21, 2013

HII NI BAADHI YA VIDEO YA TUKIO KWENYE SHAMBULIO NCHINI NAIROB NI HATARI SANA:

Imetoka MILLARDAYO.COM
Ni dhahiri kwamba ndugu zetu wamepata tabu sana kwa tukio hili, ni shambulio ambalo limefanya idadi ya waliofariki kufikia 39, hizi video mbili zinaonyesha baadhi ya matukio wakati wa uokoaji nje na ndani ya Westgate Mall ambapo Polisi wamesema ni zaidi ya watu 600 wameokolewa kutoka ndani.
TOA MAONI YAKO HAPA:

Thursday, September 19, 2013

DAY 2: PICHA ZA BEHIND THE SCENE ZA FILAMU YA CLOUD 112 INAITWA "DR MAX" HIZI HAPA;

Habari za leo wadau wangu wakubwa wa blog hii pamoja na filamu zangu, hopefull mko vizur SANA , na mimi nipo mzima wa afya Alhamdulilah, Bado tupo Kambini kwa ajili ya kuendelea kuishoot Filamu ya "DR MAX" kwa ajili yenu, Na Leo kama tulivyo ahidiana tutakua tukipeana picha za nyuma YA Pazia Kwa kile kinachoendelea huku, kila tutakapo kua wazima wa afya kwa mtindo wa DAY, Juzi niliweka picha na ilikua ni  DAY 1, Leo kwa taratiibu kabisa nime wawekea picha za DAY 2, Jinsi tunavyoshoot huku:
Karibu sana kuziangalia picha za DR MAX behind the scene DAY 2: Hizi hapa....

Wednesday, September 18, 2013

LULU AMEFANYA FILAMU MOJA NA MAMA KANUMBA, CHECK HILI KAVA NA ALICHOANDIKA:

Mwigizaji wa sinema za Kibongo,Elizabeth Michael(Lulu) amecheza filamu na mama wa aliyekuwa msanii wa Bongo Movies,marehemu Steven Kanumba,Frolah Mtegoa iitwayo Mapenzi ya Mungu ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

 Lulu amepost kava la filamu hiyo kwenye mtandao wa instragram na kuandika kuwa …MAPENZI YA MUNGU....ELIZABETH MICHAEL + FLORA MTEGOHA(MAMA KANUMBA)....STAY TUNED …..
Huku baadhi ya watu wakimpongeza na kumwambia hope 448 hongera mungu azid kukuangazia .amani yake iwe juu yako,

 Hii ni mara ya kwanza Lulu kufanya filamu na Mama Kanumba tangu alipopata matatizo ya kesi ya mauaji ya msanii Kanumba na pengine kuibua maswali kwa mashabiki ni nini kimeongelewa ndani ya filamu hiyo kati ya mtu na ‘........’.
 Filamu hiyo pia imemshirikisha msanii wa Bongo Fleva,Linna Sanga.
TOA MAONI YAKO HAPA:

JOANITA ARUDI KWA KISHINDO NA FILAMU YA HARAKA YA NDOA!

(Habari / Picha: Na Ripoti Filamucentral / FC)
MWIGIZAJI wa kike Bongo Fatuma Makame ‘Joanita’ anakuja na filamu inayojulikana kwa jina la Haraka ya Ndoa, Joanita ni moja kati ya mazao ya mtayarishaji na muongozaji wa kitambo Mussa Banzi msanii huyo ambaye ni mahiri katika uigizaji anaamini kuwa moja ya sababu inayokwamisha wasanii ni mfumo wa usambazaji kwa sasa anakuja na kampuni nyingine ya usambazaji............

Tuesday, September 17, 2013

VIDEO YA MAELEZO NILIYOTOA JUU YA FILAMU YANGU MPYA YA ''DR MAX'';

Nimepata Comment zenu kupitia Twitter account yangu pamoja na Facebook fanpage, ya kua mnataka maelezo mafupi juu ya ujio huo wa filamu mpya, kwa vile nawapenda na kuwajali na pia najali na mnachoniambia kuomba km mashabiki zangu, nimeaka hii hapa video fupi yenye maelezo ya kueleweka kuhusu Filamu mpya ya ''DR MAX'' ni kwa ajili yenu tuu;
AHSANTE
TOA MAONI YAKO HAPA:

BAADHI YA PICHA ZA BEHIND THE SCENE ZA FILAMU YANGU MPYA INAYOITWA DR MAX HIZI HAPA;

Kwanza sina budi kumshkuru M/mungu muumba wa kila kitu, kwa kutueka wazima mpaka muda huu mimi wewe pamoja na wengine, Pili niwashkuru sana nyinyi Fans wangu  kwa kuendelea kuniunga mkono katika kazi zangu takriban zote ninazozitoa, kwasababu nyinyi ndio mnaonifanya nitengeneze Filamu nzuri kila siku, Sasa baada ya kufanya vizur kwa Filamu ya SHAHADA kwa msaada wenu. Ndugu yenu nimeingia kambini,na sasa natengeza Filamu nyengne kwa ajili yenu, filamu hiyo inaitwa DR MAX, kwa ushirikiano wenu nina imani DR MAX itakuja kuleta mapinduzi makubwa ya Filamu Tanzania, hii ni DAY 1 ambayo nimeamua kukuekeni picha za kinachofanyika na pia tutaendelea kupeana picha mpaka siku tutakayo maliza kwa mtindo wa day 1, day 2 mpaka tutakapo maliza tuombe uzima tuu;
 PICHA ZA DR MAX behind the scene DAY 1 ni hizi zifuatazo:-

Monday, September 16, 2013

SABABU 6 ZILIZOANDIKWA, ZA KWANINI TAMASHA LA FILAM LA DAR NI MUHIMU TANZANIA KULIKO ZIFF:

(Habari / Picha: Na Fred Bundala / BONGO5)

Kwa muda mrefu tamasha la filamu la kimataifa la filamu Zanzibar, ZIFF limekuwa likifanyika kwa ufanisi na maandalizi makubwa ya kuvutia. Hatuwezi kubeza umuhimu wa tamasha hilo kwa Tanzania hasa kwa jinsi ambavyo hukutanisha filamu za kimataifa, watu muhimu kwenye kiwanda cha sinema duniani na jinsi tamasha linavyoitangaza Tanzania na kivutio cha watalii.
Lakini licha ya kuwa na mafanikio makubwa na kuhusisha wadhamini wengi, ZIFF si tamasha linaloweza kutoa mchango wa moja kwa moja wa maendeleo ya filamu za nyumbani. Tamasha hilo limekuwa sehemu iliyotawaliwa na uzungu mwingi na kuzifanya filamu za Tanzania kuwa mtoto aliyegeuzwa wa kambo kwenye familia ya wazazi wake mwenyewe.
Huenda ujio wa Dar Filamu Festival, DFF unaweza ukawa mkombozi kwa filamu za Kiswahili za hapa nyumbani. Ndio tamasha linalohitajika zaidi kwanza ili kuzipa nafasi zaidi filamu za nyumbani zishindane zenyewe kabla ya kushindanishwa na zile za kimataifa.
DFF Linaweza kuonekana dogo kwakuwa ndio linaanza, lakini kwa muda mrefu Tanzania ilihitaji jukwaa moja kubwa kama hili la kujivunia filamu zetu (hivyo hivyo zilivyo) na kuwafanya watu wazipende na kuthamini vyao kwao.
Hizi ni sababu kwanini tamasha hilo ni

NISHA AWAPIGA TAFU WASANII CHIPUKIZI KIMTINDO HUU HAPA;

MSANII wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ jana aliendesha zoezi la kuwafanyia usahili wasanii chipukizi ambapo alikuwa akitafuta wasanii 50 kwa ajili ya kufanya nao kazi katika kampuni yake ya Nisha’s Film Production.Zoezi hilo lilifanyika katika ukumbi wa Vijana, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo majaji waliokuwa wakiwafanyia usahili wasanii hao ni, Wastara Juma, Idrisa Makupa ‘Kupa’ Jimmy Mafufu, Benny Kinyaiya na Nisha mwenyewe.
(Habari / Picha: Na Gladness Mallya / GPL)
TOA MAONI YAKO HAPA:

Sunday, September 15, 2013

MATOKEO YA LIGI KUU YA VODACOM: JKT RUVU YAONGOZA LIGI, SIMBA WASHIKA NAFASI YA PILI

Simba SC 2 - 0 Mtibwa Sugar
Mbeya City 1 - 1 Young Africans
Kagera Sugar 1 - 1 Azam FC
Coastal Union 0 - 0 Tanzania Prisons
Ruvu Shooting 1 - 0 Mgambo JKT
JKT Oljoro 1 - 1 Rhino Rangers
Ashanti United 0 - 1 JKT Ruvu


Kwa matokeo haya JKT Ruvu Stars inaongoza ligi kuu kwa kufikisha pointi 9 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 7 na Ruvu shooting yenye pointi 6..


imetoka blog ya SHAFFIHDAUDA
TOA MAONI YAKO HAPA:

Friday, September 13, 2013

HIVI ULIIONA ILE VIDEO YA VURUGU BUNGENI ILIYOWEKWA ONLINE TAREHE 05/SEPT/20013 NA ITV:



TOA MAONI YAKO HAPA:

DUUH!!!! STORY NZIMA YA KUFUMANIWA NA MKE WA MTU YA MZEE NGURUMO HII HAPA:

 From GLOBALPUBLISHER:
Stori: Brighton Masalu
SIKU chache baada ya kustaafu muziki, mwanamuziki mkongwe nchini, Maalim Mohamed Gurumo ‘Mzee Gurumo’ amekiri kupitia maisha mabaya ujanani ikiwemo kufumaniwa na mke wa mtu pamoja na uvutaji wa ‘sigara kubwa’ Ijumaa linaanika.

Akizungumza katika mahojiano na Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Runinga ya East Africa chini ya Mtangazaji, Salama Jabiri mwanzoni mwa wiki hii, Gurumo alisema miongoni mwa mambo mabaya ambayo hawezi kuyasahau maishani mwake ni pamoja na hayo.
KUFUMANIWA:
Katika sakata hilo, Gurumo alisema kuwa ilikuwa ni mwaka 1961 ambapo alikuwa na uhusiano na mke wa mtu ambaye aligoma kumtaja, ndipo siku moja wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo ‘wakiponda kirauli’ ghafla walisikia hodi na ndipo mwanamke huyo alipomwambia kuwa anayegonga mlango ni mumewe.
“Niliogopa sana, ikabidi nijibanze nyuma ya mlango, alipoingia tu...............

REGINALD MENGI AJIBU MAPIGO, AKANA UFISADI:

 IMETOKA HABARI LEO:
MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi amejibu tuhuma zinazosambazwa kwa lengo la kumchafua katika jamii, zikimhusisha na ufisadi kwenye sekta za madini, gesi na mafuta. Pamoja na majibu ya shutuma hizo, Dk Mengi amesisitiza kuendelea na azma ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria waliohusika na uchafuzi huo, ili sheria ifuate mkondo wake.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Dk Mengi alisema hajapata kufanya udalali katika vitalu vya madini kama tuhuma hizo zinavyodai.
Alisema shutuma kwamba anafanya udalali katika vitalu vya madini na kuwa anajiandaa pia kufanya udalali katika vitalu vya mafuta na gesi, alizipokea kupitia barua pepe aliyotumiwa Septemba 7 na mtu aliyejitambulisha kama ‘CCM Tanzania’.
Alisema pamoja na..............

MOVIE MPYA YA CHOPA NA MISS TANZANIA 2011 SALHA ISRAEL TAYARI WAMESHAINGIA LOCATION KUSHOOT;

IMEANDIKWA BONGO5
Chopa na Salha
Chopa ameshare picha akiwa na mrembo huyo kwenye Instagram na kuandika: Tajir Chopa Mchopanga kaopoa miss tz.. On set na salha Israel, my new film.”
Hiyo sio filamu ya kwanza Salha kuigiza kwani tayari ameigiza kwenye movie ya kampuni ya RJ Company iitwayo, Bud Luck akiwa na waigizaji wengine kama Batuli na Johari.
“Kufanya movie ilikuwa ni moja ya ndoto zangu kubwa. Nilikuwa na mawazo kwamba hata ningeshindwa kupata taji la Miss Tanzania basi ningeingia moja kwa moja kwenye uigizaji. Lakini ilinibidi nisubili kidogo baada ya kushinda taji lile na muda ndio huu umefika,” gazeti la Mwananchi April mwaka huu lilimnukuu.
TOA MAONI YAKO HAPA:

Thursday, September 12, 2013

SANDRA ATOA WOSIA WA KIFO:

GLOBALPUBLISHER
 Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu za Kibongo, Salma Salmini ‘Sandra’ ametoa wosia kuwa siku akiaga dunia azikwe siku hiyohiyo, maiti yake isilazwe.

Akizungumza na paparazi wetu, Sandra alisema alishawaambia ndugu zake pamoja na mumewe kuwa siku akiaga dunia azikwe haraka kwani imani yake inasema hivyo pia babu yake alimhusia hivyo.
Mwigizaji huyo alisisitiza kuwa, hata kama akiaga dunia asubuhi basi azikwe mchana kwa sababu familia yao ina asili ya Kiarabu mtu akifa anatakiwa kusitiriwa haraka iwezekanavyo kwani kuichelewesha maiti ni kuiongezea adhabu.
“Nimeshawaambia ndugu zangu na mume wangu kwamba ikitokea nimekufa maiti yangu isisubiri ndugu, jamaa na marafiki, hata kama mume wangu akiwa hayupo nizikwe tu,” alisema Sandra.

TOA MAONI YAKO HAPA:

ROBIN VAN PERSIE AMPITA BERGKAMP KWA MABAO UHOLANZI - BADO MAWILI AMFIKIE KLUIVERT;

ROBIN VAN PERSIE amemfunika gwiji wa soka wa Uholanzi Denis Bergkamp kwa kufunga mabao mengi katika listi ya washambuliaji wa nchi hiyo walioifungia The Oranje mabao mengi.

Van Persie anakaribia kuwa mfungaji bora wa muda wote kwa taifa lake.

Mabo yake mawili aliyofunga jzui yamefanya ampite mchezaji mwenzie wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkamp mwenye mabao 38, wakati Van Persie akiwa na mabao 38.

Van Persie sasa anashika nafasi ya pili nyuma ya Patrick Kluivert, ambaye ana mabao 40, na sasa kwa hakika ni suala la muda tu kabla ya Van Persie kumfikia na kumpita mshambuliaji huyo wa zamani wa FC Barcelona.

Mshambuliaji huyu wa Manchester United alifunga goli la kwanza akiwa na jezi ya Uholanzi mnamo mwaka 2005, alipoweka kimiani goli la nne katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Finaldn katika michuano ya kugombea kufuzu kucheza kombe la dunia 2006.

imetoka SHAFFIHDAUDA
TOA MAONI YAKO HAPA:

(VIDEO)MADAM WEMA SEPETU AKIIMBA TAARABU, ASSU NA NYIMBO ZINGENE ANGALIA UTOE COMMENT:


TOA MAONI YAKO HAPA:

Wednesday, September 11, 2013

BABY MADAHA ASAINI MKATABA WA T.SH MILLION 50 NA MENEJA WA MR NICE:

  From BONGOMOVIES:
Mwanadada anayefanya vizuri sana kwenye muziki na filamu,baby Madaha amelamba bingo ya uhakika na kampuni ya Candy n’ Candy Records Label ya jijini Nairobi iliyomsainisha mkataba msanii mwingine wa Tanzania Mr.Nice hivi karibuni.
Akizungumza kwa simu na bongomovies leo meneja wa msanii huyo  Joe Kariuki amesema kuwa  pamoja na msanii huyo kupewa mkataba huo wa million hamsini (50) pia wamempa mwanadada huyo gari ya kutembelea ya kisasa aina ya AUDI TT (pichani) na nyumba  kali mitaa kijitonyama jijini  Dar es salaam.
Pamoja na hayo pedeshee huyo wa Mr.Nice ambaye ndio mmiliki wa studio hiyo amesema wanataka kumuhamishia msanii huyo jijini Nairobi nchini Kenya kwa kipindi cha mwaka mmoja ili afanye nao kazi huko kwani wamegundua kuwa anakubalika sana nchini humo na wapenzi wa muziki.
Baby madaha ambaye  anatarajia kutua nchini leo akitoka Nairobi pamoja na meneja wake kwa ajili ya kuachia video ya  wimbo wake wa kwanza aliofanya na Label hiyo uitwao (Summer Holiday) ambao umefanywa huko huko jijini Naironi: TOA MAONI YAKO HAPA:

DUUUH!!! DIAMOND PLATNUMZ ASEMA KUANZIA LEO HATAKI COLLABO NA MTU YOYOTE KIBONGO BONGO;

Baada ya maneno mengi kutoka kuhusiana na ngoma mpya ya msanii DIAMOND PLATNUMZ, ameamua kuondoa ukimnya na kusema  kuhusiana na wote waliyosema kuibiwa ngoma hiyo kina mna moja ama nyengne,Diamond alifunguka leo alipokua akifanya interview na radio ya cloudFm jijini Dar- es - salaam,. Lakini pia  licha ya Diamond kukanusha madai hayo ambayo yalitolewa na Dayna na,Baba levo,Pia  alifika mbali na kusema kuanzia sasa hataki Collabo na mtu yoyote, ni bora afanye mwenyewe na wala hataki mtu aje amwambie anataka  Collabo labda kwa watu ambao anaheshimiana nao atafanya nao, lakini wengne wengine wasahau kabisa collabo na yeye,

Pia alielezea suala la kua na mtoto au kumtia mimba mwana denti wa FORM 4, kua suala hiyo c kweli na wala hana mtoto, laiti angekua nae asingemtelekeza angemfikisha kwa mama naseeb kisha baaas:
Hizo ni skando tuu za kutengenezewa na watu lkn hazina ukweli wowote ule: TOA MAONI YAKO HAPA:

HUU NDIO MJENGO WA MADEE MSANII WA BONGO FLEVA TANZANIA ULIYOMALIZA HIVI KARIBUNI:

Msanii wa bongo fleva T.Z HAMAD MADEE ameshare picha ya mjengo wake, ambao anaamini kuwa bila ya mziki pengine labda asingekua nayo so haina budi kushkuru mungu, madee amesema ngoma yake ya POMBE YANGU imesaidia sana kufanikisha kuimaliza ngoma iyo kwa sababu imempatia show nyingi sana na za ela ndefu,
Madee amesema nyumba iyo ipo maaneo ya Mbezi ya Kimara jijini Dar-es - salaam ambayo kwa sasa imemaliza kabisaa bado kuhamiwa tuu;

Kumbe BONGOFLEVA  inalipa kiasi hichi:
TOA MAONI YAKO HAPA:

(VIDEO) HII HAPA VIDEO YA DENTI AKIELEZEA MKASA MZIMA MPAKA KUPATA MIMBA YA DIAMOND:


TOA MAONI YAKO HAPA:

Tuesday, September 10, 2013

ELIZABETH MICHAEL "LULU" ACHAGULIWA KUWA BALOZI WA "DAR FILAMU FESTIVAL"



Dar Filamu Festival Idara Habari Maelezo jana
 Ikiwa ni wiki moja imepita toka mwigizaji mrembo wa Bongo Movie Elizabeth Michael aka Lulu azindue filamu yake ya ‘Foolish Age’ katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam milango yake ya mafanikio imeendelea kufunguka.>

Kupitia akaunti yake ya Instagram @Hotlulumichael, ameweka picha akiwa na waandaaji na kutoa shkurani zake kwa kuchaguliwa kuwa Balozi wa ‘Dar Filamu Festival’.

“Shukrani za dhati kwenu DAR FILAMU FESTIVAL kwa kunichagua kuwa BALOZI wenu(OFFICIAL ACTRESS 2013/2014)…”


Lulu kwa sasa anafanya shughuli zake za filamu chini ya kampuni ya Proin Promotions.
Dar Filamu Festival (DFF) ni tamasha la filamu linalotarajiwa kufayika kwa siku tatu kuanzia (September 24-26) katika viwanja vya posta-Kijitonyama, Dar es salaam. Kwa mujibu wa filamucentral, tamasha hilo litaambatana na utoaji wa Semina kwa wadau wa filamu, kuonesha filamu za kitanzania kwa watu wote bure na kutakua na filamu nne kwa siku kuanzia saa kumi na mbili jioni mpaka saa tano usiku.
Story imetoka MTANDAO wa BONGO5:
TOA MAONI YAKO HAPA:

PICHA ZA MAZISHI YA MSANII WA BONGO MOVIE HAPA MAENEO YA MAKABURI YA KINONDONI:

JENEZA LA MAREHEMU ZUHURA MAFTAH   
Marehemu Melisa alikua  ni msanii wa bongo muvi ambae jana habari zilitufikia kua ameaga dunia, Maremu MELISA alifahamika kwa mara ya kwanza kwenye filamu ambayo alifanya na mimi CLOUD 112, ilikua inakwenda kwa jina SECURITY, Marehemu Melisa pia alikua ni miongoni mwa vipaji ambavyo niliviibua mm, kama itakumbukwa licha ya kuwemo kwenye hiyo filamu pia ilikua ni filamu yake ya kwanza:
Kwa ambao hawakumbuki wakiangalia tena filamu ya SECURITY ni mwanadada ambae mwanzoni uwanja wa Ndege ZANZIBAR anakutana na mimi,( cloud 112),huku ana mtoto wote wakiwa wanasubir ndege kuelekea DAR-ES-SALAAM:
Marehemu ameacha mtoto mmoja;
kwa sasa hivi Mimi pamoja na wadau wengine tulifika kwenye maziko yake, kusindikiza mwenzetu kwenye makaazi yake ya milele M/mungu ailaze roho ya maremu Mahali pema Peponi Amin;
ZIFUATAZO NI PICHA ZA HAPA MAENEO YA MAKABURI YA KINONDONI:

SPORT: SAMUEL ETO'O ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA - KOCHA WAKE ASHINDWA KUTHIBITISHA KAMA KWELI AU HAPANA

Kocha mkuu wa Cameroon Volke Finke amekataa kuthibitisha kwamba nahodha wa timu hiyo ya taifa Samuel Eto'o amestaafu kuichezea timu hiyo. Mchezaji huyo mpya wa Chelsea ambaye ni mshindi wa mara nne wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, ameripotiwa kuwaambia wachezaji wenzake kwamba mechi ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Libya ndio ilikuwa ya mwisho kwake.
Ushindi dhidi ya Libya umewafanya 'Simba Wasioshindika' kufuzu kwenda kucheza play off kwa ajili ya kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia 2014.
"Samuel Eto'o ni mchezaji mzuri na ni vizuri ingekuwa yeye ambaye angezungumzia habari hizi. Yeyey ndio anaojua maamuzi yake," Finke alisema.


"Ameitumikia vizuri timu ya taifa na ndio maana ingekuwa vizuri angemzungumza mwenye kuhusiana na suala hili."
Eto'o, ambaye alijiunga na Chelsea kutoka klabu ya Anzhi Makhachkala mwezi uliopita, hakuhudhuria mkutano wa baada ya mechi kuthibitisha juu ya taarifa za kustaafu kwake.Lakini kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vya mchezaji huyo ni kwamba Eto'o anataka kuweka umakini wake katika kukiendeleza kituo chake cha kufundishia soka.
Eto'o pia kwa sasa ndio analipa fedha matibabu yote ya kocha wa zamani wa timu hiyo ya taifa Jean Paul Akono, ambaye alipata kiharusi mapema mwaka huu. 
By SHAFFIHDAUDA TOA MAONI YAKO HAPA:

SOMA HII IMEANDIKWA KUHUSU MELI ZINAZOSAJILIWA ZANZIBAR JINSI ZINAVYOICHAFUA TANZANIA :

 IMETOKA  HABARILEO:
UDHAIFU wa Sheria ya Mamlaka ya Usafiri wa Baharini ya Zanzibar (ZMA) ya mwaka 2006, umeichafua Tanzania katika usafiri wa majini duniani, baada ya sheria hiyo kutoa nafasi ya kusajiliwa ovyo kwa meli za kimataifa bila udhibiti.
Kutokana na udhaifu huo, Tanzania imejikuta ikiwa na meli 400 zinazopeperusha bendera yake duniani, zikiwamo mbovu, zilizouzwa na zilizoondolewa sokoni.
Uchunguzi wa gazeti hili, umebaini si meli ya mv Gold Star pekee iliyokamatwa na bangi tani 30 yenye thamani ya Sh bilioni 125 hivi karibuni, iliyochangia kuchafua jina Tanzania, bali kumekuwa na meli zingine zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali duniani.
Udhaifu
Mamlaka ya Usafiri wa Baharini ya Zanzibar (ZMA) imekuwa ikisajili meli kupitia wakala wake wa usajili ambaye ni kampuni ya Philtex ya Dubai.
Utaratibu huo, ulianzishwa baada ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujitoa kwenye Sheria ya Usafiri wa Majini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2003, na kuunda sheria yake ya Usafiri wa Bahari ya Zanzibar ya mwaka 2006 ambayo pia...

Monday, September 9, 2013

(VIDEO) MOVIE TRAILER YA ELIZABETH MICHAEL LULU "FOOLISH AGE" ANGALIA HAPA:


TOA MAONI YAKO HAPA:

BEKI WA TIMU YA YANGA MBUYU TWITE AVAMIWA NA WEZI USIKU MNENE:

Na Joan Lema na Hans Mloli wa GPL: CHAMPIONI
 
BEKI wa Yanga, Mbuyu Twite (pichani), amevamiwa na wezi nyumbani kwake usiku mnene na kukombwa vitu vingi vya ndani.
Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa beki huyo raia wa Rwanda maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumamosi.
Taarifa zinasema kuwa, Twite hakuhudhuria mazoezi siku iliyofuata katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola jijini Dar kutokana na tatizo hilo.
Mchezaji mmoja wa Yanga ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema ni kweli beki huyo ameibiwa vitu vya ndani, lakini akasisitiza kwamba hajui ni vitu gani na vina thamani ya kiasi gani.
Championi Jumatatu lilipomtafuta Twite kuzungumzia suala hilo alikiri kweli ameibiwa lakini

(OFFICIAL VIDEO) CHIDI BENZ FT NONINI - GET DOWN:


TOA MAONI YAKO HAPA:

HIZI PICHA: KWA WASIO MFAHAMU MAREHEMU ZUHURA MAFTAH (MELISA) WA BONGOMOVIE KWA JINA:

Habari zilizotufikia  zinasema kuwa mwigizaji wa bongo movies Zuhura Maftah  ama  Malisa (Pichani) amefariki dunia leo hii.
Mpaka blog hii inaingia mitamboni Bado hatujaweza kupata taarifa kamili za chanzo cha  kifo chake ila tunafanya juhudi kuweza kuzipata na tutawaletea  zitakapokuwa tayari.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
 hizi zifuatazo ni baadhi ya picha zake marehemu MELISA:

Sunday, September 8, 2013

(OFFICIAL VIDEO) JUX - UZURI WAKO:


TOA MAONI YAKO HAPA:

(SPORT)BAADA YA KUFUNGWA NA GAMBIA - KIM POULSEN ASEMA TAIFA STARS ILISTAHILI KUFUNGWA:

Taifa Stars imemaliza vibaya mechi za mchujo za Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika baada ya kufungwa na Gambia huku Kocha Kim Poulsen akisema timu yake imefungwa mabao mepesi.
Wenyeji Gambia wameshinda mabao 2-0 katika mechi hiyo iliyochezwa leo (Septemba 7 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Independence ulioko hapa jijini Banjul ukiwa ni ushindi wake wa kwanza katika kundi hilo la C ambapo imemaliza ikiwa ya mwisho ikiwa na pointi

(PICHA)MUONEKANO WA ANTY EZEKIEL TANGU ATOKE HOSPITALI KUTIBIWA MKONO:

Msanii wa filam nchini T.z ANTY EZEKIEL ameshare picha ake baada ya kutoka hospital na zinazomuenesha yuko fiti san sana, Aunty Ezekiel alipigwa chupa na kujeruhiwa vibaya na mwanadada aliyetambuliwa kwa jina la Ivony wiki chache zilizo pita, na hizi ni baadhi ya picha zake zinazomuonesha akiwa fresh na mzima wa afya:
                                                                                  
check picha zingine hapa-:

WENGI MASKINI KWA SABABU HAWATUMII FURSA ZILIZOPO:

IMEANDIKWA HABARILEO:
MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi amesema Watanzania wengi wanazidi kuwa masikini kwa sababu hawazitumii fursa za utajiri uliopo nchini, hivyo kutaka vijana kuona kwa macho fursa hizo ili waweze kujikwamua kutoka kwenye dimbwi hilo la umasikini.
Akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa washindi watatu wa shindano la nini kifanyike kuzalisha ajira nyingi hapa nchini aliloanzisha Mwenyekiti huyo wa IPP, Mengi alisema baada ya Watanzania kupofushwa kuwa nchi yao ni masikini, wengi walibweteka na kushindwa kuchangamkia fursa zilizopo hali ambayo imeifikisha nchi hapa ilipo.
Alisema jambo la msingi kwa vijana wa Tanzania ni kuibua mawazo ya shughuli gani atafanya badala ya kukimbilia namna ya kupata mitaji, kwani wengi ambao wamekimbilia kutafuta mitaji wamejikuta wanaipata mitaji hiyo, lakini wakashindwa namna ya kuitumia.
Washindi katika shindano hilo ambalo limeanzishwa na Mengi lijulikanalo kama Tweet Bora ni Lilian Wilson wa Chuo Kikuu cha Ardhi aliyepata Sh milioni moja, Susan Senga ambaye ni mfanyabiashara ndogo alipata Sh 500,000 na Ombeni Kaaya ambaye ni mjasiriamali kutoka Nzega, Tabora aliyekabidhiwa Sh 300,000.
Katika maoni yao, Lilian alipendekeza kuwa ili kuondoa tatizo la ajira wajasiriamali waliofanikiwa na Serikali waanzishe mifuko ya kuwekeza mitaji kwenye biashara za vijana zenye uwezekano wa kukua haraka badala ya kutegemea mikopo ya benki au taasisi za fedha.
Susan Senga yeye alipendekeza kuanzishwe vipindi maalumu kutoa elimu ya ujasiriamali ya kuwawezesha vijana kuwatoa katika fikra ya kuishi kutegemea ajira ili kujiairi.
Kwa upande wake, Ombeni Kaaya katika maoni yake alisema tafiti wanazofanya wanafunzi wa elimu ya juu mwaka wa mwisho zihusu jinsi watakavyojiajiri katika fani zao kwani itasaidia wengi wajiajiri.
Naye Dk Donath Olomi wa Taasisi ya Management and Entrepreneurship Development ambao ndio wanaoteua washindi, alisema katika shindano la mwezi huu jumla ya maoni 979 yalipokewa na watachagua washindi watatu kutoka katika maoni hayo.
TOA MAONI YAKO HAPA:

HII NDIO MELI YA TANZANIA ILIYOKAMATWA NCHINI ITALY NA SHEHENA YA DAWA ZA KULEVYA :

Meli iitwayo Gold Star imekamatwa karibu na pwani ya Italy ikiwa na zaidi ya tani 30 za dawa za kulevya ambapo Polisi wa Italy wamesema documents zinaonyesha ilisajiliwa Tanzania.
Taarifa nyingine ya polisi imesema mzigo huo una thamani ya pound millioni 50 ambayo kwa pesa za kitanzania ni kama 126,582,278,481 na meli yenyewe ilikua na timu ya watu tisa ambao wanatoka Egypt na Syria na mzigo wote wameupakia kutoka Uturuki.
Unaambiwa baada ya kuona mchezo wao umefahamika, watu waliokuwemo kwenye meli waliamua kuanza kuichoma moto meli hiyo na wote tisa walijirusha baharini kwa nia ya kutaka kukimbia lakini wakakamatwa mapema tu na kukutwa na hizo dawa za kulevya aina ya hashish ambazo thamani yake inagonga kwenye £50m.
Bandari husika ya Italia walipewa taarifa kwa siri mapema siku kadhaa kwamba meli hii ilikua imebeba tani nyingi za dawa za kulevya hivyo wakawa wanaifatilia kwa siku kadhaa kabla ya kuikamata.
Msemaji wa bandari amesema hawakutegemea kama meli hiyo ingekua imebeba kiasi hicho cha dawa za kulevya na pia hawakutegemea kama watu waliokuwemo ndani yake wangeichoma moto ili kupoteza ushahidi japo zoezi hilo halikufanikiwa na dawa zikaonekana.
Meli hiyo imesogezwa kabisa mpaka kwenye bandari na moto umezimwa huku msako zaidi ukiendelea kwenye sehemu nyingine za meli hiyo ili kuona kama kuna dawa nyingine za kulevya huku watu wote tisa wakiwa wanaendelea kuhojiwa.
HABARI HII Imetoka millardayo.com

TOA MAONI YAKO HAPA:

Monday, September 2, 2013

(OFFICIAL VIDEO) DIAMOND PLATNUMZ - MY NUMBER ONE:


TOA MAONI YAKO HAPA:

MAZOEZI YARUDISHA MWILI WA RAY KIGOSI :

KWA wale waliokuwa wakichongachonga wanayoyajua wenyewe, watakuwa wameumbuka sababu staa wa sinema za kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameanza kupata mwili kama zamani.

 Kudhihirisha kama mwili wake umeanza kurudi kama zamani, paparazi wetu alimnasa staa huyo katika uzinduzi wa video ya wimbo wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, My Number One uliofanyika katika Hoteli ya Serena, Posta jijini Dar na kuona mwili wa staa huyo ulivyojengeka…

CHADEMA KUZOA WASANII WA BONGO FLEVA WAMO PIA MASTAA WAKUBWA:

IMEANDIKWA NA  HABARI LEO:
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeendelea kuwavuta wasanii kujiunga na chama hicho, ambapo sasa wasanii wanne wa muziki wa kizazi kipya, maarufu Bongofleva na filamu, wanatarajiwa kutangazwa kuhamia chama hicho wiki hii. Wasanii hao wanadaiwa tayari kukubali kuingia kwenye chama hicho na wanatarajiwa kutangazwa rasmi hadharani katika mkutano wa hadhara utakaofanyika jijini Dar es Salaam.
Kukubali kwao kuingia katika siasa, kunatajwa kutokana na ushawishi mkubwa uliofanywa na wabunge vijana wa chama hicho, pamoja na Diwani wa CCM kutoka kata moja ya Wilaya ya Kinondoni, ili chama hicho kivune kura za vijana katika uchaguzi mkuu wa 2015.
Wabunge hao wa Chadema na majimbo yao katika mabano ni Halima Mdee (Kawe); Kabwe Zitto (Kigoma Kaskazini); John Mnyika (Ubungo) na Joseph Mbilinyi, jina la kisanii Sugu (Mbeya Mjini).
Habari kutoka kwa watu wa karibu na wasanii hao pamoja na ndani ya Chadema, zinawataja wasanii hao kuwa ni......

Sunday, September 1, 2013

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA KAMPUNI YA SHELL ZAINGIA MAKUBALIANO, UWEKEZAJI WA SECTA YA MAFUTA NA GESI:

Mh. Ramadhan abdalla shaaban na  Bw.Alex Knospe
IMETOKA MICHUZI BLOG:
Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kampuni ya Royal Dutch Shell plc (shell) kwa pamoja wametangaza uwekaji saini wa Waraka wa Makubaliano.

Waraka huo unaweka bayana ushirikiano kati ya Kampuni ya Shell na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar katiaka secta ya Mafuta na Gesi na inafafanua hususani kuhusu hatua za awali zinazohusiana na kujenga uwezo katika secta ya mafuta na gesi pamoja  na maendeleo ya vijana katika kukuza ujuzi wao kwenye secta hii, ikiwa ni pamoja najitihada za elimu na uwezo wa ujasiria mali.

Axel Knospe, mwenyekiti wa shell deepwater Tanzania alieleza kuwa, kampuni ya shell ina nia ya kuwa na uhusiano imara na serikali ya zanzibar na pale itakapofaa, itaanza hatua za utafiti amabao utafanyika kwa njia endelevu,ya kiuchumi, kijamii na inayowajibika kimazingira.

Kwa upande wake wazir wa Ardhi,Nyumba, Nishati wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mh. Ramadhani Abdalla Shaaban alisema kuwa utiaji saini wa waraka huo ni hatua kubwa inaoyoonesha jitihada za serikali za kuendeleza secta ya Nishati Zanzibar.  
TOA MAONI YAKO HAPA:

HII HAPA NYIMBO YA DAYNA ANAYOSEMA AMEIBIWA NA DIAMOND PLATNUMZ (NUMBER ONE)

Juzi kati mkali wa music wa BongoFleva Diamond Platnumz alizindua rasmi ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la My Number One katika ukumbi wa Serena Hotel ambao watu wengi mashuhuri walialikwa kwenda kuiona video hiyo,
Kubwa lililoibuka kwa sasa ni kutoka kwa msanii wa kike wa Bongofleva pia, Dayna Nyange (Dayna), ameibuka na kusema kua wimbo ule ni wa kwake na msanii Diamond ameuiba, kwa mujibu wa Dayna anasema, Alimpelekea Diamond demo ya wimbo huo ili kuangalia uwezekano wa kumshirikisha lakin kadri siku zilivyokua zinakwenda Diamond alioneka kua bize sana, na mwisho wa siku, ngoma ndo iyo iliyozinduliwa juzi.
Licha ya hayo kikubwa na cha kushangaza ni kwamba Producer wa ngoma iliyozinduliwa ni SHEBY CLEVER na wa hii ya DAYNA ni huyo huyo, Je unafikiri kuna ufanano wowote kwenye ngoma izo;Hebu isikilize hii demo ya Dayna huku ukisubiri rasmi ngaoma hiyo ya diamond Kisha Utatuandikia maoni yako hapo chini kwa upande wako unahisi vip???:

TOA MAONI YAKO HAPA: