Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Saturday, August 31, 2013

BONDIA FRANCIS CHEKA ATAWAZWA KUWA BINGWA WA NDONDI DUNIANI:

IMETOKA GAZETI LA HABARI LEO:
BONDIA bora nchini, Francis Cheka ametawazwa kuwa bingwa wa dunia katika uzito wa kati, baada ya kumpiga bondia wa Marekani, Phill Williams katika pambano lililochezwa usiku wa kuamkia jana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa mchezo huo. Ubingwa huo unatambuliwa na Shirikisho la Ndondi Duniani (WBF).
Cheka alipanda ulingoni saa 5.30 usiku, akifuatiwa na Williams dakika sita baadaye na ilipofika saa 5.38, mgeni rasmi wa mpambano huo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete, alipanda ulingoni na kuwasalimia mabondia hao.
Akizungumza baada ya kutambulishwa kwa mabondia hon, Dk Mukangara mbali na kuwatakia heri, alimtaka Cheka kupambana kwa lengo la

VIDEO:MSANII BATULI AKIELEZEA MAMBO MBALI MBALI KUHUSIANA NA FILAMU T.Z:

Yobnesh Yussuph maarufu kama BATULI ni mmoja kati ya wasichana wanaofanya filamu hapa nchini Tanzania.Weekend hii alionekana katika uzinduzi wa Filamu "FOOLISH AGE" ya msanii mwenzake  Elizabeth Michael (Lulu), Batuli alipata kupiga story mbili tatu na Mtandao wa BONGO5 kuhusiana na Mipango, Mikakati, pamoja na Changamoto alizonazo katika tasnia hii ya Filamu Tz hasa ukizingatia kua yeye ni mrembo pia:
Angalia mahojiano hayo kwa njia ya Video:
TOA MAONI YAKO HAPA:

KIKUNDI CHA WAASI CHA M23 CHACHAKAZWA VIBAYA:

 IMETOKA GAZETI LA HABARI LEO:
"KIKUNDI cha waasi cha M23 kinachopambana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kimeripotiwa kupigwa vibaya na kutikisa nguvu za kikundi hicho kutokana na baadhi ya wapiganaji wake kuripotiwa kupoteza maisha.
Mapigano baina ya M23 na Jeshi la Serikali ya DRC linalosaidiwa na Kikosi Maalumu cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO), yameibuka upya ndani ya wiki hii.
Habari za kiintelijensia ambazo gazeti hili limezipata zinasema kuwa, kutokana na shambulio hilo, Serikali ya Rwanda imelazimika kuingilia kati kusaidia waasi hao kwa kupeleka bataliani mbili zenye jumla ya askari 1,700 huko DRC, ili waweze kukabiliana na nguvu ya majeshi ya DRC, Monusco na Brigedi ya Majeshi ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa yenye mamlaka ya kujibu mapigo (FIB).
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, Rwanda imepeleka bataliani hizo mbili zenye askari 850 kila moja saa 24 zilizopita na kwamba wamevuka mpaka kuingia DRC katika eneo la Kibumba, lakini wanashindwa kusonga mbele.

HIZI NDO SABABU ZA AUNTY EZEKIEL KUPIGWA CHUPA CLUB BILICANAS:

Jumapili iliyopita katika ukumbi wa bilicanas mwanadada, Aunty Ezekiel alipigwa chupa na kujeruhiwa vibaya na mwanadada aliyetambuliwa kwa jina la Ivony Bigirwa katika show ya muziki ambapo wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliopo chini ya kampuni  ya Wema Sepetu ya Endless fame walikuwa wakitambulisha nyimbo zao mpya
Chanzo nini?

PICHA ZA BEHIND THE SCENE FILAMU YA SHAHADA KUTOKA CY&CL COMPANY

 Baada ya kufanya vizuri katika filamu ya TOBA kampuni ya CY & CL Company, imekuja na filamu nyingine ambayo itakuja kushika kasi. Filamu hiyo ni SHAHAADA ambayo, kazi yake imeshaanza na hivi sasa picha zake zimekuwa zikisambaaa na kuzua maswali mengi juu ya filamu hiyo. angalia behind the scene za filamu hii hapa hapa: lkn pia usisahau kuacha Maoni yako;

(PICHA)ANGALIA PICHA ZA UZINDUZI WA MUVI YA ELIZABERTH LULU MLIMAN CITY

Kwa mara ya kwanza jana muingizaji muigizaji wa filamu bongo ELIZABERTH MICHAEL  (LULU)  alizindua FILAMU yake iliyokua ikisubiriwa na wengi sana, "FOOLISH AGE" pale MLIMAN CITY ,uzinduzi ulifana vilivyo hasa pale ilipoimbwa wimbo wa  Lady Jide "YAHAYA" zifuatazo ni baadhi ya picha katika uzinduzi huo: