Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Thursday, April 18, 2013

Hapa ndipo alipolala Bi Kidude

 Hii ndiyo safari ya mwisho ya mwanamuziki nguli wa muziki wa mwambao, Fatuma Bint Baraka maarufu kama Bi Kidude.


Wednesday, April 17, 2013

Bi Kidude Afariki Dunia

Aliyekuwa nguli wa muziki wa mwambao Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, Bi Kidude amefariki dunia leo hii. Taaarfi zaidi kuhusiana na mkongwe huyo.

Saturday, April 13, 2013

Hivi ndivyo wasanii walivyomkumbuka Kanumba

  Baada ya wasanii wa Bongo Movie kumaliza kusali misa na kupita makabulini kwa marehemu Steven Kanumba walirudi wote Leaders Club, kwaajili ya kuangalia uzinduzi wa filamu ya mwisho wa nguli hiyo. Katika filamu ili ambayo iliandaliwa na Jack Wolper na kuzinduliwa na mama Kanumba na meya wa manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda.

 Wageni kutoka Ghana, waliudhulia ili kuonyesha ni jinsi gani walivyokuwa wakimkubali msaniii huyo mpaka kuamua kuja katika kumbukumbu yake.














Filamu ya mwisho ya Kanumba yatoka

Hii ndiyo filamu ya mwisho ya swahiba wetu Steven Kanumba ambayo imetoka jana ya the Love & Power

Bob Junior kumalizia matamasha Ulaya

 Nyota wa muziki wa kizazi kipya mabye kwasasa anafanya matamasha yake katika nchi ya Ulaya, Bob Junior amesema matamasha hayo ndiyo yatakuwa matamasha yake ya mwisho kabla ya kurudi jijini Dar es salaam

Sunday, April 7, 2013

Bongo Movie wazuru kaabuli la Kanumba

 Wasanii mbalimbali wa Bongo Movies leo walikutana kwaajili ya siku maalum ya kumbuka msanii mwenzao marehemu Steven Charles Kanumba. Katika siku hiyo ambayo iliambatana na missa fupi iliyofanyika kanisani, na baadaye kufika makabulini kwaajili ya kumsomea dua, kisha wasanii wote watakutana Leaders 'Club kwaajili ya uzinduzi wa filamu ya mwisho ya msanii huyo. Mungu ailaze roho ya marehemu Kanumba mahala pema peponi... AMIN














Balaa la filamu ya Selo

 Hizi ndio picha za filamu mpya ya SELO, ambayo inatarajiwa kuja hivi karibuni chini ya kampuni ya Cy & Cy Company chini ya Cloud 112. Kwa upande wa filamu hii, ni miongoni mwa filamu ambzo zimetulia katika matukio makali na yenye mchanganyo wa picha wa kisasa. Hebu angalia baadhi ya picha za Scene za filamu hiyo ambayo inaongozwa na Cloud 112.
 Hapa Big Matovolwa akiwa na Cloud 112, na kwa mbaaali Libert, wakijiandaa kuingia on Set.

 
 Big akiwa na mwanadada Janny, ambaye alifanya kazi nzuri sana katika filamu ya Selo.
 Kazi ilifika hadi kwenye ofisi za Tbc, ambapo napo makamuzi yaliendelea kama kawaida ili kuleta uharisi... hebu angali picha hizi kisha uniambie....










 Sasa hapa ndipo mtu anapoingia ndani ya Selo, ili kujua nini kilimfanya kuingia ndani ya Selo hebu fuatilia filamu hii pindi itakapo toka hivi karibuni.

 Kuna muda wa kufurahi kidogo, hapa ni Cloud 112, China Zaholo, Beka Makuka, Libert Msuya, Zakalia Baruti na mwanadada Janny.





 China akitafakari jambo baada ya kusomewa Scene yake....