Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Monday, January 28, 2013

Lulu apata auheni

MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata dhamana leo baada ya kukidhi masharti aliyowekewa na mahakama.
Dhamana hiyo imetolewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya hoja za mawakili wanaomtetea kukubalika.
Masharti aliyokuwa amepewa ni pamoja na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali wenye kiasi cha Sh. milioni 20 kila mmoja na kuwasilisha pasi ya kusafiri ya msanii ili kutotoka nje ya nchi hadi kesi hiyo itakapokamilika.
Huku mashabiki wake na baadhi ya wasanii wenzake wakiwa na furaha mahakamani hapo, kila mmoja alisikika akisema Mungu mkubwa.

Wasanii walipoamua kujitokeza kuchangia Ofisi Dar Live


 Siku ya jumamosi ya majuzi wasanii wa filamu wote walikutana katika viwanja vya Dar Live katika tamsha la Siku ya Masuper Star Lengo kubwa lilikuwa kujenga urafiki na mashirikika mengine pamoja na kukusanya fedha zitakazo saidia kujenga Ofisi ya hadhi ya shirikisho la Wasanii maarufu kama TAFU chini ya raisi wa shirikisho hilo Simon Mwakifamba.  Katika tamasha hilo pia walimwarika Meya wa Ilala Jery Slaa, huku wasanii wenyewe ndio wakiwa watoa burudani wakubwa katika tamasha hilo
















Wasanii wacharukia maandamano


Wasanii wa filamu leo walikuwa kwenye kikao maalum kwaajili ya kuendelea kujadilia masuala ambayo yameendelea kuikumba tasnia hiyo, katika kudai haki yao ya kumiliki kazi zao, na kuomba baadhi ya viongozi katika Bodi ya filamu Tanzania kuweza kuachia ngazi kutokana na kuwa kikwazo katika kutafuta haki zao. Wasanii hao walisisitiza kama hawatapata nafasi nzuri ya kuweza kukaa pamoja na waziri na kumweleza mambo yao, basi wataanzaisha maandamano makubwa ya nchi nzima kuhakikisha baadhi ya viongozi wa Bodi ya Filamu wakitoka.





 Baadhi ya wasanii walitaka wasanii wenyewe kwa wenyewe kwanza lazima waadabishane ilikuweza kuonyesha kwamba ufuatiliaji wa mambo yao yanakuwa ya kiuhakika na wa kufuata sheria kama inavyotakiwa. Hata hivyo baadhi wengine walidai kwamba, wapo wenzao wamekuwa kikwazo kwa kutofika katika kikao hicho, na kusababisha kuzoletesha nguvu ya mapambano dhidi ya maadui zao.









Tuesday, January 22, 2013

Fid Q atunikiwa cheti, kwa kutoa elimu ya Albino


Mkali wa muziki wa Hip Hop nchini Farid Kubanda 'Fid Q' ametukiwa na cheti na afisa mtendaji mkuu wa taasisi ya Under the Same Sun, Mr Peter Ash kutokana na kujitolea katika mapambano dhidi ya unyanyasaji wa walemavu wa ngozi na kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na walemavu wa ngozi ambao wanajulikana zaidi kama Albino.
Fid Q anasema Mr Peter ambaye pia ni mzungu albino alimtunukia cheti hivyo cha CERTIFICATE OF APPRECIATION, kutokana na kulidhishwa na mapambano na elimu aliyoitoa kwa jamii kuhusiana na ulemavu wa ngozi.
Alisema mapambano hayo yalikuwa zaidi katika mikoa ya kanda ya ziwa. Pia alisema ataendelea kutoa elimu kwa jamii na kuwaelimisha kwamba jambo hilo linaweza kutokea kwa jamii yoyote.

Bob Junior atapa mtoto wa kiume

  Nyota wa muziki wa kizazi kipya Rummy Nanji 'Bob Junior' ameuanza mwaka vizuri kwa kufunga ndo na mpenzi wake, mwanzoni mwa mwezi huu na hatmaye hii leo tunazungumza msanii huyo amepata mtoto wa kiume.  Mwanamuziki huyo pia hivi karibuni alikuwa akimalizia video ya wimbo wake wa Kichumu, ambao umekuwa wakati furaha za harusi na sasa kupata mtoto. Bongo Unit inampa pongezi raisi wa Sharobaro kupata mtoto huyo.



Saturday, January 19, 2013

The Finest ya Mwana Fa yaja


TAFF yaomba wasanii kujitolea


  Shirikisho la wasanii Tanzania 'TAFF' leo limefanya kikao ili kuweza kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuendesha shirikisho hilo, kutokana na upungufu wa fedha walizokuwa nazo. Raisi wa shirikisho hilo Simon Mwakifamba, alisema shirikisho hilo halitegemei fedha kutoka Serikalini hivyo ni juhudi zao pekee ndizo zinazoweza kufanikisha kwao. Alisema pia sheria mbalimbali zimekuwa zikiwabana, hivyo huu ni wakati wa wao kuungana na kushikamana ili kuweza kupamba juu ya ufisadi wanaofanyiwa, kwenye tasnia yao kuanzia kwenye sheria ambao inawapa nafasi kubwa Wasambazaji kuwa na haki.
 
 Pia aliwataka wasanii kugangamala na kuungana pamoja ili kudai haki zao, katika kikao kilichofanyika Vijana, Kinondoni.
 Baadhi  ya wasanii wakiwa kwenye kikao
 Mkono na mwenzake, wakisikiliza kikao kutoka Al Riyam Production.
 Dr Cheni akiwa na Dino
 Steve nyerere akisikiliza mkutano
 Jack Wolper akiwa na wasanii wengine wakishikana mikono kuashirikia mshikamano



Wednesday, January 16, 2013

Matata apata ajali

Mwigizaji wa filamu wa Rashidi Waziri Matata amepata ajali ya kugongwa na gari leo na kuumia vibaya sana hadi kupelekea kupelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kulazwa katika wodi ya Sewa hadi 18. Taarifa zinadai msanii huyo kwa sasa amekatwa mguu mmja kutokana na ajali hiyo. Wasanii wote wanaombwa kwenda kumuona na kumsaidia msanii mwenzao kwa kile kilichomkuta, kwani kabla hujafa hujaumbika.

Dully Syskes ajisafisha kesi ya Arafat Ngumijiwe

Mwanamuziki wa kizazi kipya Dully Syskes ameomba radhi mashabiki wake kutokana na kitendo alichokifanya aliyekuwa rafiki yake wa karibu Arafat Ngumi jiwe cha kumnajisi mtoto wa kiume. Dully alisema hana uhakika kwa hilo ila amekiachia  chombo cha dora kuweza kutekeleza wajibu wake na ataonekana na hatia basi sheria  mkondo.
Amesema kuomba kwake  radhi kunatokana na mtu huyo kuwa rafiki yake wa karibu, jambo ambalo ameona bora kufanya hivyo ili kuepukana na kashfa hiyo.

Fungate yaja kufungua 2013 ndani ya Cy & Cl company


 Katika kuanza mwaka kwa kasi kampuni ya CY & CL Company, inakuja na filamu mpya na yakisasa zaidi ya FUNGATE, filamu ambayo haijawahi kutokea katika ujio wa filamu wa kisasa. Fungate ni miongoni mwa filamu za kisasa ambazo zinakuja kuleta mabadiliko, huku akiongozwa na Issa Mussa 'Cloud 112', Libert Msuya, Batuli, na wengine wengi ambao kwa sasa wanafanya vizuri kwenye tasnia hii.

 



Saturday, January 5, 2013

Jakaya akamilisha safari ya mwisho ya Sajuki

 Raisi wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete jana amekamilisha katika safari ya mwisho ya msanii wa filamu nchini Juma Kilowoko 'Sajuki'katika makabuli ya kisutu jijini Dar es salaam. Katika mazishi hayo yaliyofanyika muda wa saa saba yaliudhuliwa na viongozi mbalimbali, pamoja na wasanii wengine kutoka tasnia mbalimbali kuhakikisha wanakamilisha safari ya mwisho ya msanii huyo ambaye ameteseka kwa muda mrefu kutokana na maradhi ya uvimbe.
 Msanii Cloud 112 akitoa maelekezo juu ya kuusogeza mwili wa marehemu karibu na kabuli, kwaajili ya kumstiri ndugu Sajuki.
 Angalia picha zaidi za mazishi ya Sajuki