Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Wednesday, October 17, 2012

NSSF watoa vitambulisho kwa wasanii


Leo wasanii wa filamu nchini walikusanyika pamoja katika semina maalum ambayo ilikuwa ikitolewa na Shirika la Hifadhi ya mfuko wa kijamii la NSSF. Mkurugenzi uendeshaji wa kampuni hiyo Crescentius Magori, alisema shirika hilo limeamua kufanya hivyo baada ya kugundua Watanzania wengi wakiwemo wasanii ambao hawajaajiliwa wamekuwa wakikosa fulsa ya kujiunga na mfuko huo. Alisema mara nyingi watu walioajiliwa ndiyo wamekuwa na nafasi kubwa ya kupata huduma zitolewazo na mfuko huo ikiwemo huduma ya matibabu, kiinua mgongo na huduma zingine ambazo zinatokana wanachama wa mfuko huo. Aidha alisema lengo la mfuko huo waajiliwa na wasiokuwa waajiliwa kuweza kupata huduma hiyo, lakini mwamko umekuwa mdogo sana kwa watu waliojiajili.
Swebe pamoja na Sudi





Recho

Raisi wa shirikisho akiongea Mwakifwamba


Maya

 

Batuli

Tuesday, October 16, 2012

Matonya amchukua Kingwendu kuwa densa

Nyota wa muziki wa kizazi kipya Matonya, amesema hivi sasa ameamua kuwachukuwa wachekeshaji kwaajili ya kuwafanya Madensa, pindi anapopanda jukwaani kuimba. Alisema anafanya hivyo lengo lake lake likiwa ni kutimiza ahadi yake ya kutoa burudani mbili kwa wakati mmoja. Alisema miongoni mwa stedi shoo wake, ni Kingwendu, na wengine.

Wasanii washerekea Nyerere Day Sunrise

 wasanii wa filamu nchini ambao wanaunda kampuni ya Nyerere The Power, juzi walikuwa wakisherekea Nyerere Day katika beach ya Sunrise. Katika sherehe hiyo ambayo pia ilionyeshwa filamu ya Mwalimu Nyerere, wasanii waliweza kujiburudisha kwa kuogelea huku kiongozi wa kundi hilo Steve Nyerere akitoa burudani ya kuimba.
 Stive Nyerere


 Steve Akiwa na Mr Kupa
 Mr Zungu akiwa na simu kibao



 Mambo yalikuwa namna hii

Tino kutoa ofa uzinduzi wa O.C.D

MSANII maarufu wa filamu nchini,  Hissan Muya ‘Tino’, amesema ,  WALE WENYE VIPAJI WOTE VYA SANAA YA MAIGIZO NA NYINGINEZO ZOTE SIKU YA TAR 26 october KWENYE
UZINDUZI WA TINO ,,,,,TINO MUYA FILMS.... ITAZINDUA MUVIE YA C,I,D PIA ITAZINDUA RASMI ,,,,,,MUVIE STAR SEACH,,,,YANI M,S,S,,,,,,,NJOO UJUE UTAAANZIAAA WAPIII KUONYESHA KIPAJI CHAKO,,,,,,,,,,UKUMBI BISNESS PAK VICTORIA
Akizungumza hivi karibuni Tino alisema kuwa kwa sasa amesitisha mpango wa kutengeneza na kucheza  filamu za mapenzi kwa kuwa wengi wamejikita kutengeneza filamu za aina hiyo na  kusahau mambo muhimu yanayoigusa jamii hasa janga kubwa la ukimwi, njaa na mengine mengi.

Tino alisema sababu nyingine ya kuzitosa filamu za mapenzi ni baada ya kutengeneza filamu  ya ‘Shoga’ na baadaye kubadilishwa jina na kuitwa ‘Shoga yangu’  iliyokuwa na lengo la kuelimisha jamii kuhusu suala zima la ushoga, badala yake ikaja kumletea matatizo.

Cpwaa na Ay wazindua video ya kuhamasisha kupigiwa kula Channel O


Nyota wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini ambao wanawania tuzo za Channel O, Ambewe Yesaya 'Ay' na Cpwaa, wamezindua video maalum kwaajili ya kuhamasisha upigaji wa kula katika tuzo wanazowania nchini afrika kusini.
Cpwaa akitoa maelezo ya kutosha jinsi ya kuwapigia kula.