Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Friday, August 17, 2012

Milion 2 atakaye mkamata mbanaji Cd Feki za Bongo Movie

Wasanii wa filamu leo kwa pmaoja walikutana katika viwanja vya Leaders Cloub kujadili juu ya hatma yao na maslahi yao katika tasnia hiyo na juu ya watu wanaobani Cd za filamu zao na kuuza kama njugu. Pia makundi mawili ambayo yalikuwa yakikizana siku zote kati ya kampuni inayojiita Bongo Movie chini ya mwenyekiti Jb na shirikisho la filamu nchini chini ya Saimon Mwakifamba, wamemaliza mgogoro wao huku kila mmoja akiweka ahadi kwa mwenzake kwamba anatambua uwepo wake. Miongoni mwa migogoro ambayo ilifanya mpasuka huo kuwa mkubwa pale Mwakifamba alipofika kwenye Tv fulani na kutangaza kwamba Bongo Movie haitambui kwa mujibu wa sheria,  huku akianika baadhi ya picha zinazoashiria kundi la Bongo Movie kwamba ndilo linaua tasnia kwa kufanya umalaya. lakini siku ya leo tofauti zote hizo waliziweka chini, na kuibua hoja mpya kwamba ni jinsi gani wanaweza kupambana na maharamia ambao wanadurufu kazi za wasanii na kuwafanya wawe mafukara daima. Miongoni mwa matukio ambayo walikubaliana kuyafanya ni kufanya maandamano makubwa yakiongozwa kwa kuvaa Tisheti, za kuashiri kupamba na uadui huo wa kudurufu kazi za wasnii. Huku wasnii mbalimbali wakitoa dau ili kukamilisha maandamano hayo, miongoni mwa watu waliotoa michango yao ni  Cloud 112 alitoa shilingi elfu 50, na usafiri wa kuelekea kwenye maandamano, Jb altoa laki moja, Tues Kinagala alitoa shiling laki moja na mengine wakasema watajua na kampuni yake cha kufanya, Dk Cheni alisema yeye atatoa usafiri, wakati wakubwa wao na wasambazaji wakubwa hapa nchini STEPS ENTERTAIMENT wakitoa ofa kwamba yoyote atayefanikisha kupatikana kwa mwaharamia mmoja basi atachukua donge nono la MILIONO MBIL . Kazi hiyo vijana wa mjiniii























Tuesday, August 14, 2012

TBL chini Gland Mult yafutulisha wasanii

 Kampuni ya biaTBL  inayozalisha kinywaji cha Gland Multa, leo walikuwa wakifutulisha wasanii na wadau mbalimbali wa kampuni hiyo. Mkurugenzi wa masoko wa kampuni hiyo, Mr Fimbo aliwataka wadau wote kushirikiana, hususani wasanii na wadau wengine wa kampuni hiyo. Wasanii mbalimbali wa Bongo Movie waliudhulia ghafla hiyo, akiwemo Cloud 112, Jb, Hatman, Aunt Ezekiel pamoja na wasanii wengine.
 Antie Ezekiel akiwa kwenye futari, baada ya kujiunga na uislam na sasa anafunga.

 Jacob Stephan akipata futari
 Cloud 112 akipata futari
 Hatman na Jb
 Mkurugenzi masoko wa bia ya kilimanjaro, George Kavishe



Antie na Cloud nje hoteli wakati wakijiandaa na kuondoka

penzi la Kiza mwisho wa matatizo

 Baada ya kufunika katika filamu ya kidini ya TOBA, kisha sasa kutoka na TRIPLLE L, kampuni ya  Cy & Cl Company, inakuja na filamu ya kichawi ambayo haikuwahi kutokea hapa nchini ya PENZI LA KIZA. Ni filamu ambayo imejaa matukio ya ajabu ambayo yamekuwa yakisumbua jamii kila kukicha. Ni filamu ambayo ni ya kishirikina, iliyobeba mandhari ya kimapenzi. Huenda ikawa filamu ya kichawi na ya kusisimua kuliko filamu zote zilizotoka mwaka huu, na hata kama ipo basi huenda isifike katika kiwango ambacho filamu hii ilifikia. Ni ya kisasa, na yenye mvuto wa aina yake..... Si ya kuikosa namba moja na mbili ni PENZI LA KIZA.

Super Nyamwela ala shavu Finland

 Nyota wa muziki wa dansi katika unenguaji, Super Nyamwela amekula shavu nchini Finland ambapo walikwenda kufanya show na kugewa offa kwamba atakuwa anagewa mkataba kwaajili ya kwenda kufundisha chuo cha unenguaji kilichopo nchini humo.Nyamwela alisema ofa hiyo, alipewa baada ya kufika huko na  kuanza kuwafundisha wazungu katika chuo kikuu cha nchi hiyo, ambacho kinajihusisha na utamaduni hususani wa kiafrika. Alisema aliwafundisha  zaidi ya wiki mbili alikuwa akitoa mafunzo kwa wazungu hao juu ya kucheza nyimbo za afrika, na baadaye kumwambia kwamba muda wowote na saa yoyote wanaweza kumwita tena nchini humo kwaajili ya mafunzo zaidi.
 pia kiongozi wa bendi hiyo Ali Choki alisema hivi karibuni anatarajia kuzindua albamu yake katika sikukuu ya Idd, na kutangaza jina la albamu hiyo ambayo itaakuwa na nyimbo saba.
 Banza Stone pia aliongeza kwa kusema, baada ya kuzinduliwa kwa albamu hiyo atatunga wimbo mpya

Monday, August 6, 2012

Machapa watatu wajipanga kivyao


BENDI ya dansi nchini ya Mapacha Watatu, kuondokewa na mwanamuziki wao Kalala Junior, wameachai wimbo mpya wa Ona Naonewa huku wakijiandaa na ujio wa albamu yao ya pili.
Mmoja wa wanamuziki wa bendi hiyo Jose Mara, alisema kwamba wimbo huo wamemshirikisha Ali Kiba pamoja na Kharidi Chokoraa utakuwa kwenye albamu hiyo ambayo itakuwa na nyimbo 7.
Aidha alisema kwamba jina la la albamu hiyo, amemwachia Chokoraa kwakuwa albamu ya kwanza alishatoa yeye jina, pia alishatuka wimbo kama usio wa baba na huu wa Ona naonewa.
“Ujue kupeana nafasini jambo la muhimu, hivyo jina  la albamu hii itatoka katika wimbo ambao atautunga yeye” alisema.
Pia alisisitiza kusema bendi hiyo, haitachukua mwanamuziki mkongwe kuogopa lawama, ila itachukuwa wanamziku chipukizi.

Miliki wa Twanga Pepeta akana kuongelea bendi na Ramadhan

Mmiliki wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka, amekana kwamba hakuongea lolote na  gazeti lolote kuhusiana na bendi yake ya Twanga Pepeta la  kuhusiana na jinsi inavyoendelea na ratiba yake katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani Kareem. Asha alisema hataki kugombanishwa na dini yake,  na  magazeti kwakuwa yeye ni muislam kamili. Aidha amesema yanayoandikwa kwenye magazeti hayo, yeye wala hausiki na hajawahi kuongea, kwani anaamini atakapoongelea suala hilo  atakuwa anakiuka maadili. Mwisho  amedai kwamba hayo yote atakuja kuongelea baada ya mfungo wa Ramadhani Kareem  huu kuisha.

Bonface atoka na Mike tee

BAADA YA KIMYA KIREFU TANGU AACHIE ULE WIMBO WAKE WA “ULISEMA” AKIMSHIRIKISHA MIKE TEE (MNYALU) AMBAO ULIFANYA VIZURI KWENYE VITUO MBALIMBALI VYA REDIO NA TELEVISION. BONYFACE A.K.A HANDSOME BOY…A.K.A KIDUME  BAADA YA KUHAMA MJI WA MOROGORO NA KUHAMISHIA SHUGHULI ZAKE ZA MUZIKI HAPA DAR TAYARI AMEACHIA WIMBO MATATA SANA UNAOKWENDA KWA JILA LA “BADO MTOTO” KAZI MZIMA IKIFANYWA CHINI YA PRODUCER MACHACHARI MENSEN SELECTA KUTOKA STUDIO ZA STUD DEFFETARTY.  AKIWA CHINI YA LEBO YA MENSEN SELECTA DEFFETARTY MUSIC. BONYFACE PAMOJA NA PRODUCER WAKE  WAPO CHIMBO KUPAKUA MAWE MENGINE AMBAYO YATAACHIWA HIVI KARIBUNI. USHAURI NA MAONI JUU YA WIMBO HUU, UTAPOKELEWA KWA MIKONO MIWILI NA KWA HAMASA KUBWA ILI KUKUZA MUZIKI WETU WA HAPA TANZANIA. KWA MAWASILIANO ZAIDI NA MSANII MWENYEWE ANGALIA PROFILE YAKE HAPO CHINI :
NAME                         :          BONFACE MATEZA
JINA LA KISANII       :           BONY FACE
WIMBO                        :           BADO MTOTO
STUDIO                       :           STUD DEFFETARTY
MTAYARISHAJI        :           MENSEN SELECTA

Saturday, August 4, 2012

Stive Nyerere akamilisha Get Out

Filamu mpya ya Stive Nyerere ya Get Out, ambayo imemalizika leo, filamua ambayoimebeba mastaa kibao akiwemo Shemsa Ford, Sinta na wengine wengi.

Kupa, Ali






Faridi Uwezo akitoa maelezo ya jinzi gani watu wanavyotakiwa wawe Location