Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Wednesday, February 29, 2012

Mjumuishe mwenzio pia kujua Taarifa zilizomo humu

kwa kuwa kuna wadau wengi wanaoonekana kufuatilia Taarifa mbalimbali katika Blog Yangu na Pia wana marafiki wengi ambao wapo mbali kidogo na Taarifa za Bog hii nimeamua kuwaletea urahisi wa kumshirikisha pia mwenzio akiwa katika FACEBOOK kwa kumtumia Habari ambayo umekutana nayo humu kwa kutumia

SEND BUTTON


Ambayo itakuwezesha kumtumia mtu mojakwamoja kwenye facebook Account yake (Facebook Wall Page) na kujua taarifa za INJINI ya jiji


au


LIKE BUTTON


Kitufe ambacho kitaonesha kuwa wewe umeipenda taarifa katika Blog yangu na kuwajulisha watu wengine kama umependezewa na Taarifa husika

BUTTON zote za SEND na LIKE zinapatikana katika kila Taarifa ninayokuletea (POST) kwa chini yake


AKHSANTE kwa ushirikiano!!


Tuesday, February 28, 2012

JERAHA LA MOYO ipo mitaani

CY & CL kwa kushirikiana na Steps Entertainment ilikuandalia Filamu kali inaoitwa Jeraha la Moyo ambayo kwa muda mrefu mlikuwa mnaisubiri kwa hamu sasa IPO MITAANI.


Kwa taarifa za haraka haraka toka iingizwe sokoni filamu ya Jeraha la Moyo imeonekana kupokelewa kwa mwitikio Chanya ambapo wadau na wapenzi wa filamu nchini wanonekana wakinunua kwa wingi nakala zake.

Filamu hii imeshirikisha wasanii maarufu na wakali wa sanaa nchini akiwemo Kajala Masanja, Elizabeth Swinny, Zamaradi Salumu, Zuwena Mussa, Marry Mtemi pamoja na Injini ya jiji  CLOUD 112.

Kama bado hujapata nakala yako nakushauri uende katika stoo zetu na upate nakala yako. Akhsanteni kwa ushirikiano wenu na Mchango wenu.

Haluuuuuaaa!!!

Arsenal yagoma kutumia Fedha zaidi katika usajili ujao


Mtendaji mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis amesisitiza kwamba Klabu haitopagawa kiasi cha kutumia pesa nyigi katika dirisha kubwa la usajili la wachezaji baada ya kutangaza kupata faida ya pauni milioni 49.5(£49.5million ) kwa mwaka siku ya jumatatu.

Faida hiyo, £46.1m imetokana na uuzaji wa wachezaji, ikijumuisha na kumuuza Cesc Fabregas kwa £30m, Samir Nasri kwa 24m na Gael Clichy kwa £7m.

Cloud 112 alilifahamu kama wiki mbili zilizopita ya kuwa Arsene Wenger alipanga bajeti yapata £55m ili kukisuka upya kikosi chake kwa kuongeza wachezaji wapya katika kipindi cha usajili wa majira ya joto ingawa inaonekana kuna uwezekano wa kuwauza baadhi ya wachezaji wake katika kikosi cha sasa hivi.

Mjerumani Mario Gotze na Lukas Podolski wanaonekana kutakiwa zaidi na wenger katika kuongeza makali ya kikosi chake

Target: Mario Goetze    Wanted: Lukas Podolski

pia inaonekana anaweza kuhamishia biashara yake kwa chelsea kumnyakua kinda la Kiingereza Daniel Sturridge na Fowadi ya Anderlecht Matiaz Suarez. Lakini Gazidis amesema klabu itaendelea kuangalia matumizi yao. "Kikubwa ni kuangalia tunafanya nini tukiwa kwenye uwanja", kama alivyosema Gazidis.

Monday, February 27, 2012

CY & CL inawapa pole STEPS Entertainment


Siku ya ijumaa ya tarehe 23 mwezu huu Steps Entertainment ilikutwa na Msiba wa mmoja wa wanafamilia yao ambapo Mazishi yalifanyika siku ya Jumatatu maeneo ya wilaya ya Kinondoni Viktoria.

 Cy & Cl inawapa pole Kampuni ya STEPS Entertainment kwa kukutwa na msiba mzito kama huo na Kuwaombea kwa Mwenyezi mungu awape faraja na Amani katika kipindi kigumu kama hiki.

Mwenyezi Mungu alitoa na ametwaa, tunajua kama Sisi tulimpenda sana ila Mungu ndiye aliyempenda zaidi yetu.


Sunday, February 26, 2012

Toba na Triple L zapamba moto

Msanii maarufu jijini Issa mussa Khamis (Cloud 112 kama alivyozoeleka) amekaa vyema kwa mwaka huu kuhakikisha kwamba Kazi zake zote za Filamu zinaenda sawia katika Tasnia ya Filamu Nchini.

Kwa kukutanabaisha hilo harakaharaka amekuandalia filamu  kali Tatu ambazo anahakikisha kwamba hutochoka kuangalia kazi zake za filamu nchini.

TOBA:

Filamu ya TOBA imeshutiwa Bamba Beach kwa umakini mkubwa na kuhaririwa na Kampuni ya Digital Art Production Chini ya usimamizi wa Said Mangush na amethibitisha kwa kuhakikisha kwamba atahakikisha filamu inakuwa babu kubwa.

TRIPLE L:

Triple L imeshutiwa na E-Media kwa kushirikiana na Cy & Cl Company ambayo imewashirikisha wasanii wakali kama Patcho Mwamba, Cloud 112 mwenyewe na wengine kibao.